TANGU KALE NA MAWZO YA NDUGU JOHN MWAKILAMA


    
kuanzia miaka ya 2000 hasa hasa 2002 hivi baada ya filamu ya girlfriend iliyoandaliwa na George tyson na kuchezwa na wanamuziki GK,TID na na waigizaji wengine kama Monalisa,Ndende,Sauda kilumanga, ilipelekea mwanzo wa mtiririko wa filamu nyingi sana zilizochezwa kwa lugha ya kiswahili,na hii ilifanya filamu hizi zipokelewe kwa nguvu sana na jamii kwakua jamii ilikua imekwisha choshwa na filamu nyingi za kina Mofe Damijo,Peter Edochie toka Nigeria ambazo ziliteka soko hapa nchini, hivyo ujio wa filamu hizi kwa lugha ya kiswahili ulibadirisha mtazamo wa watazamaji, swali ni je kwanini ziliitwa filamu za kiswahili? kunaweza kua na sababu nyingi kidogo lakini nadhani cha kwanza ni kuwa filamu hizi zilibebwa sana na lugha ya kiswahili, 


mbili ukosefu wa utaalam wa kutosha katika filamu hizi katika stori ulifanya watu wasikumbuke stori zake au jina la filamu husika hivyokuishia kuita filamu za kiswahili, hiyo iliendelea kwa kasi ikisaidiwa na michezo mbalimbali ya kiswahili katika televisheni zetu ambapo baadae wale waigizaji wa michezo ya televisheni (tamthilia ndo jina lake hasa lakini kwakua sisi twaigiza ndo maana hata neno maigizo linaleta maana) wakavamia hizi filamu, kwahiyo kwa muda mrefu filamu hizi zilibebwa na KISWAHILI lakini sio UFUNDI WA UTENGENEZAJI FILAMU.na nyingi zilikua ni copy and paste toka filamu za nje ila zikachezwa kwa kiswahili, wananchi walitegemea wangeona mabadiriko sasa ya kiufundi tukitumia sana msaada wa LUGHA YA KISWAHILI lakini watayarishaji wa filamu na wasanii wetu wakageuka mawe na kufanya kazi kimazoea hivyo kudharau kipengele CHA UFUNDI, mpaka leo waohawajui ni kwanini walipanda na pengine hawajui ni kwanini wanateremka kwa kasi.
Hadhira haina tena hamu ya filamu zetu imerudi kule kule tulikotoka awali.leo hii tv zetu zimejazwa na tamthilia toka nje, wasanii wanashindwa kutumia kiswahili katika filamu kwasababu hawaelewi faida yake katika soko hivyo wamevamia kiingereza ambacho kwa bahati mbaya nacho kimewashinda. hebu fikiria ni nchi ngapi zinatumia lugha ya kiswahili? na je we kama ukitengeneza filamu bora kwa lugha ya kiswahili soko lako litakuaje? LUGHA YA KISWAHILI ILIWAPANDISHA WASANII WA FILAMU WA TANZANIA LAKINI WAKASAHAU KUTUMIA LUGHA YA KISWAHILI NA UFUNDI PENGINE KWAKUWA WALIKUWA HAWAJUI KWANINI WANAPANDA KAMA NILIVYOSEMA NA SASA WANAPOROMOKA BILA KUELEWA NI KWANINI.
Haya ni mawazo yangu mimi mwenyewe. pengine niko sawa au nimekosea naamini kuwa wengine wanamawazo pia wanayoweza ongeza au kunisahihisha wanapohisi nimepotoka au kupotosha


John Mwakilama
.Posted by Bongo Film Data Base on 11:37 PM. Filed under , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for TANGU KALE NA MAWZO YA NDUGU JOHN MWAKILAMA

Post a Comment

LETS HOOK UP

.

.
.
slide

SIRI YA MTUNGI PHOTO CAPTION

Recently Commented

ALBUM YA BONGOFILM

SIMULIZI ZILIZOBAMBA KWENYE KURASA ZA KIJAMII

TAKE ONE -HBABA NA FLORA INTERVIEW

2009 Bongofilmdatabase. All Rights Reserved. - Designed by Oscar kwa ushirikiano wa SimplexDesign