TINO SASA AINGIA HATIANI.

Hisani Muya
Tino mtayarishaji na mwigizaji wa filamu Tanzania.
MWIGIZAJI Nyota katika tasnia ya filamu Bongo Hisani Muya ‘Tino’ anakuja na filamu ya kipekee kabisa inayojulikana kwa jina la Hatia (Innocent) filamu hiyo ambayo imerekodiwa katika Mkoa wa Morogoro inatarajia kuteka hisia za wapenzi wa filamu Bongo, akingea na FC mpigaji wa picha ambaye pia ni mhariri wa filamu hiyo Timoth Conrad ‘ Tico’ anasema katika kazi alizofanya kwa mwaka huu hii ni ya kipekee.

Hisani Muya
Tino akiwa location.
“Filamu ya Hatia ni moja kati ya filamu kali ambazo msanii huyu ameigiza, na Hatia ina utofauti sana katika filamu ambazo ninazifanya, kwanza tumeirekodi nje ya Jiji la Dar es salaam, katika filamu hiyo unapata mazingira tofauti ambayo tumezoea kuyaona kila siku, pia imeshirikisha wasanii wakali wenye uwezo,”anasema Tico.
Simon Mwapagata
Kapturado akiwa katika pozi.
Kisa cha filamu hiyo kinamhusu kijana INNOCENT “Tino” ambaye anakutana na vikwazo vingi katika maisha yake, kutokana na hali halisi ya maisha ya chini aliyonayo anaamua kupiga moyo konde na kuamua kukabiliana na hali iliyopo, lakini kwa bahati mbaya anaingia hatiani kwa kosa la mauaji na kukutwa na silaha kinyume cha sheria, ni hadithi yenye uzuni burudani na mafunzo.
Kulwa kikumba
Dude Muongozaji wa filamu ya Hatia.
Filamu ya Hatia inawakutanisha wasanii wakali katika tasnia ya filamu Tanzania kama vile Simon Mwapagata ‘Capturado’, Abdalah Mkumbila ‘Muhogo Mchungu’, Hisani Muya ‘Tino’, Kemmy, na Bi. Aisha, filamu hiyo imeongozwa na muongozaji mahiri wa filamu Tanzania Kulwa Kikumba ‘Dude,


CHANZO; FILAMUCENTRAL
Asante!

Posted by Bongo Film Data Base on 12:20 AM. Filed under , , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for TINO SASA AINGIA HATIANI.

Post a Comment

LETS HOOK UP

.

.
.
slide

SIRI YA MTUNGI PHOTO CAPTION

Recently Commented

ALBUM YA BONGOFILM

SIMULIZI ZILIZOBAMBA KWENYE KURASA ZA KIJAMII

TAKE ONE -HBABA NA FLORA INTERVIEW

2009 Bongofilmdatabase. All Rights Reserved. - Designed by Oscar kwa ushirikiano wa SimplexDesign