LULU AJINADI KUWA NI BIKIRA.
kituko 12:17 AM
MWIGIZAJI wa filamu Bongo mwenye umri mdogo lakini machachari katika
matukio ya mastaa Bongo Elizabeth Michael ‘Lulu’ hivi karibuni alitoa
kihoja kama si kichekesho pale alipojinadi kuwa yeye ni msichana
asiyemjua mwanaume yaani akimananisha kuwa yeye ni Bikira na hajiusishi
kabisa na wanaume.
Hata pale alipoulizwa kuhusu wanaume ambao iliwahi kuripotiwa kuwa ni
wapenzi wake, mtu kama Ali Kiba alidai kuwa ni rafiki tu wa kawaida
japo kuna wakati alidai kuwa hana marafiki wa aina yoyote.
“Unajua mara nyingi ni maneno tu ya magazeti ambayo hupenda kuniandika hivyo lakini mimi ni binti safi na sina mambo hayo ya wanaume bado mdogo mimi,”alisema Lulu.
Hata hivyo pamoja na kuongea hivyo lakini mavazi aliyokuwa amevaa yalipingana na kauli yake kuwa ni binti mwenye maadili mema, haya tena ukiyashangaa ya Mussa utayaona ya firauni.

kweli hiki ni kituko cha wiki