UUNDAJI WA FILAMU BORA NI HUU (SEHEMU YA PILI) NA CHAIBA KOMBO


Production Designer yeye ndiye msimamizi atakayeshirikiana na Director pamoja na Producer kuwachagua watu wa production crew. Halafu Director na Producer watamtafuta D.O.P, na wao ndio watakao watamtafuta Sound Engineer na Art Director.

Production Designer anaweza kushika nafasi ya Line Producer au akpaitkana Line Producer mwingine kama Sinema ina mambo mengi asije akazidiwa kazi. Director yeye ndiye msemaji mkuu kwenye production, crew yote inatii amri yake akifuatiwa na Production Manager ambaye yeye atakuwa msimazi wa production nzima ikiwemo malipo ya crew na cast halafu anakuwepo na Production Supervisor, Production coordinator, Production Secretary, First Assistant Director, Second Assistant Director, Continuity/Script Supervisor, Production Accountant, Location Manager, Unit Manager, Office Driver, Cast Driver, Equipment Driver, Security Guards na First Aid people hawa wote wakiwa chini ya Producer na Director, Director yeye ni msemaji mkuu akishirikana D.O.P. na hakuna ruhusu mtu yeyote kuwaingilia kwenye kazi yao wao ndio waamuzi wa mwisho labda Sound Engineer aone kuna hitilafu kwene wizara yake.

D.O.P. yeye anawasaidizi wkae ambao ni First Camera Operator Second Camera Operator, Gaffers, Set Runners, Light Operators.

Sound engineering yeye ni mtu wa sauti ambaye anawasaidizi wake Key Grip, Sound Mixer, Sound Technician, Boom Swinger anashirikiana na Director na D,O,P kuweka sauuti bora kwenye production.

Art Director yeye anao watu wake wengi ambayo nae ana shirikina na Directogr kuwapata naao ni; Art Designer, Costume Designer, Stunt Coordinator, Set Runners, Make Up or Hair, Wardrobe .

Na hii ndio serikali ya uandaaji mzima wa Filamu Bora wale wafadhili wanaopewa bajeti na kutoa pesa kidogo halafu baadaye kulalamika kuwa filamu imetoka vibaya hii ndio sababu, inakuwa timu haikamiliki kwani kiungo mmoja akipewa kadi nyekundu timu imeingia mashakani kufungwa, lakini timu ikikamilika matumaini ya ushindi ni asilimi miamoja.

UUNDAJI WA FILAMMU BORA

Kwanza lazima tukubaliane kuwa filamu bora hutokana na hadithi bora ambayo huandikwa kwa ufanisi mpaka kufikia mswada wa majadiliano. Halafu pia tukubaliane kuwa uandishi ni kipaji sio kila mtu akiwa msanii basi ni mtunzi.

Waandishi wako wa aina nyingi lakini mimi nataka kuongelea uandishi wa filamu ambao naona bado hapa kwetu ni tatizo kubwa. Wandnishi wa filamu hapa kwetu ni wengi ni wale walisoma aidha chuo kikuu cha Dar es salaam au chuo cha sanaa Bagamoyo. Kweli wanajitahidi kwani elimu ya sanaa wanayo lakini filamu inaundishi wake. Hebu tujiulize kwanini kila filamu tunayotoa inamapungufu kwa sababu kwanza hatuna shule maalum ya filamu nchini na pia waalimu waliobobea kwenye masuala ya filamu.Uandishi unamisingi yake ambayo hufuatwa ili kuleta maana katika haddithi husika ikiwavutia watu mwisho kufikisha ujumbe husika.

Waandishi wa aina nyingine mfano wa vitabu, habari, maigizo mengine ya jukwaa na redio wao naweza kusema wananjia pana za kufikisha ujumbe wao kwani wanaweza kuelezakwa mapana kwenye uandishi wao lakini uandishi wa filamu ni mgummu nikilinganisha na uandishi wa vitabu na maigizo ya jukwaani. Kuna dhibiti zake ambazo ukitoka nje tayari umepoteza maana ya hadithi nzima, uandishi wa filamu unavipengele vinane mpaka ufikie hatua ya mwisho (screenplay) ambaayo ndio filamu yenyewe. Vipengele hivi lazima vizingatiwe la sivyo filamu yako itakuwa na mapungufu na kuwacha watazamaji wako wakijiuliza maswali, huu ndio ugumu wa uandishi wa filamu.

Watu wengi wanaojiita waandishi hukimbilia kwenye script format ambayo wao wanona kupanga script yake kwenye mpangilio ndio tayari kamaliza lakini mswaada ni kipengere cha mwisho kabisa. Lazima tuelewe kuwa filamu haiuzwi kwenye mfumo wa mswaada kwa sababu mnunuzi hana muda wa kusoma makaratasi mia mbili kwa hiyo huwa anauziwa aidha ‘wazo’ au ‘story concept’. Kwenye masoko ya filamu watu huwa wanauza story concept na pengine story outiline. Tukubali kuwa sio lazima wewe uliyegundua wazo ndio wewe utakaye andika mswaada na kuunda filamu nzima mnunuzi anaweza kumpa muandishi mwingine aendeleze vipengele vilivyobaki.

Kwanza lazima ujichunguze kweli wewe ni muandishi au Director? Na kama ni mwandishi je wewe ni muandishi wa filamu au vitabu? Ukijijua sasa tafuta elimu ya uandishi wa filamu ambayo itakusaidia kupanua kipaji chako cha uandishi kwa ujumla kwani filamu hukupitisha kwenye uandishi mwingine ili ujue tofauti zake.

Baada ya kupata elimu ya uandishi wa filamu utaweza kuvitambua vipengele vyorte vinane.

IDEA, STORY CONCEPT, CHARACTER PROFILE, BACK STORY, STORY OUTLINE, STEP OUTLLINE, TREATMENT, DIALOGCE SCRIPT _ SCREENPLAYEWE MDAU MWENZANGU USIKOSE TOLEO LIFUATALO KUJUA NINI KINAFUATA MARA BAADA YA PRODUCER KUTAFUTA NA KUWAPATA WATU WA WIZARA HIZO KUU KWENYE UTAYARISHAJI FILAMU NA JE? KAZI IPI HASA HASA ATAFANYA NAO KUKAMILISHA FILAMU BORA YENYE VIWANGO ITAKAYO REJESHA PESA ZOTE ALIZO WEKEZA HUYU EXCUTIVE PRODUCER?!.....
Karibu sana mdau na tafadhali wafahamishe wadau wengine pia.
IMEANDALIWA NA
Chaiba Kombo
Binti WakubhubhaPosted by Bongo Film Data Base on 1:01 PM. Filed under , , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for UUNDAJI WA FILAMU BORA NI HUU (SEHEMU YA PILI) NA CHAIBA KOMBO

Post a Comment

LETS HOOK UP

.

.
.
slide

SIRI YA MTUNGI PHOTO CAPTION

Recently Commented

ALBUM YA BONGOFILM

SIMULIZI ZILIZOBAMBA KWENYE KURASA ZA KIJAMII

TAKE ONE -HBABA NA FLORA INTERVIEW

2009 Bongofilmdatabase. All Rights Reserved. - Designed by Oscar kwa ushirikiano wa SimplexDesign