HISTORIA YA BODI YA UKAGUZI WA FILAMU TANZANIA

IJUE BODI YA FILAMU TANZANIA
HISTORIA YA BODI YA UKAGUZI WA FILAMU TANZANIA
Historia ya bodi ya Filamu nchini Tanzania inaanzia kipindi cha utawala wa kikoloni ambapo mwaka 1930 Sheria ya Picha za Sinema ilitungwa na kuanza kutumika. Mnamo mwaka 1974 Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania lilitunga namba 4 Sheria ya Filamu na Michezo ya Kuigiza na mnamo mwaka 1976 na sheria hiyo ilisainiwa na rais wa wakati huo Mwalimu Julius K. Nyerere.Sheria ambayo ina tumiaka mpaka sasa. Majukumu ya Bodi ni kulinda Utamaduni kwa kuhakikisha kuwa sanaa ya filamu na michezo ya kuigiza inazingatia maadili ya Taifa.
Jukumu lake kubwa ni kukagua filamu na kanda za video,vikundi vya sanaa za maonyesho na kutoa ushauri kwa kuzingatia maadili.
Mwaka 2011 Kanuni za Sheria ya Filamu na Michezo ya Kuigiza namba 4 ya mwaka 1976 zilikamilika na kuanza kutumika. Kanuni hizo zimetangazwa katika gazzeti ya Serikali namba 156/ 2011.Kanuni hizi zimeiongezea Sheria ya Filamu uwezo wa utekelezaji.

Filamu ni Picha yoyote Jongevu. Picha Jongevu ni mpangilio wa picha ya kitu au vitu vinavyoonekana na vilivyorekodiwa katika kifaa chaochote cha kwa mfumo wa digitali,seluloid, au kwa namna yoyote ambayo picha hiyo inaweza kujongea na inajumuishapicha zilizoko katika mfumo wa filamu, video,katuni na picha zozote zinazofanana na hizo Kazi za Bodi:
Kwa mujibu wa Sheria Na. 4 ya Filamu na Michezo ya Kuigiza ya mwaka 1976, bodi ina kazi zifuatazo:

Kukagua filamu zote na kutoa ruhusa ya kuonyeshwa hadharani;
Kutoa vibali vya utengenezaji wa filamu kwa watengenezaji kutoka nje ya nchi na kusimamia utengenezaji wa Filamu zote nchini
Kukubali/kutokukubali kutoa leseni/kibali kwaajili ya kufanya shughuli za filamu au michezo ya kuigiza nchini;
Kukagua na kutoa Leseni za majumba ya sinema nchini;
Kupitisha miswada na kuratibu maonyesho ya Michezo ya kuigiza;
Kuratibu na kusimamia Bodi za Mikoa na Wilaya
Kusimamia na kuratibu utendaji wa asasi zinazojishughulisha na masuala ya filamu Nchini ( vyama,mashirikisho,asasi n.k(
Kutoa/kutotoa ruhusa ya matangazo ya filamu
Kusimamia na kuratibu utekelezaji wa Sheria ya Filamu na Kanuni zake.
Masharti mengine kwa mujibu wa sheria Na. 4 ya mwaka 1976 ya Bodi ya Filamu na kanuni zake ;
 
  KUTOKA KWENYE UKURASA WA CHOCHOTE KUHUSU FILMAU KUPITIA MTANDAO WA KIJAMII FACEBOOK 
KARIBUNI  NYOTE NA MSEME LOLOTE KUHUSIANA NA FILAMU ZETU


Posted by Bongo Film Data Base on 4:25 PM. Filed under , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for HISTORIA YA BODI YA UKAGUZI WA FILAMU TANZANIA

Post a Comment

LETS HOOK UP

.

.
.
slide

SIRI YA MTUNGI PHOTO CAPTION

Recently Commented

ALBUM YA BONGOFILM

SIMULIZI ZILIZOBAMBA KWENYE KURASA ZA KIJAMII

TAKE ONE -HBABA NA FLORA INTERVIEW

2009 Bongofilmdatabase. All Rights Reserved. - Designed by Oscar kwa ushirikiano wa SimplexDesign