LAITI WEMA AGEKUSANYA KWA KILA TOLEO LEO AGEKUWA MILIONEA HUENDA ILA ANA UTAJIRI WA....

Binti huyu hata kama akae kimya kwa kujifingia ndani bado ataandikwa tu...ila dunia ya sasa bila kuingia kwenye pillika hutakula la kuva unavyotegemea na kila aingiapo mtaani kutafuta kifuta jasho chake ndiyo kabisaaaaaaaa wazee wa rangi rangi wananenepesha mifuko yao....swalii kwenu waandishi, atakapokuja ofisini kwenu na adai asilimia ya mauzo yenu ya kila toleo lenye picha na hadithi zenye kumfedhehesha yeye hata siku nyingine hazina ukweli mtampa?!

HAYA TIRIRIKA NAYO HII UONE  IMEKAA KAA VIPI KWA BINTI MDOGO KAMA HUYU MASIKINI YA MUNGU!!

NYUMA ya sakata la Wema Isaac Sepetu (pichani) kudaiwa kufumaniwa na mume wa mtu mwanzoni mwa wiki hii, kuna siri nzito ambayo sasa imefichuka, Ijumaa lina ripoti kamili.
ISHU YASUKWA NA WASANII WENZAKE
Katika habari ya Wema kunusurika kuuawa na mwanamke huyo aliyeadaiwa kuwa ni kigogo wa Ikulu maeneo ya Mwanamboka Kinondoni, Dar es Salaam, usiku wa kuamkia Jumatatu wiki hii iliyoripotiwa na gazeti dada la hili, Risasi Jumatano juzi, imefahamika kwamba ishu nzima ilisukwa na wasanii wenzake.
WEMA AKIRI KUCHEZEWA RAFU
Akizungumza na Ijumaa baada ya habari hiyo kuwa gumzo, Wema alikubaliana na uchunguzi wa gazeti la Risasi Jumatano kuwa kuna wasanii wenzake ‘waliomuuza’ kwa lengo la kumchafua kufuatia mambo yake kuwa kwenye mstari.
NI WASANII GANI?
Hata hivyo, Wema alipotakiwa kuwataja wasanii waliocheza sinema hiyo ya bure baada ya kuwepo kwa madai kuwa anawaringishia kwa kuishi maisha ya kifahari, hakuwa tayari zaidi ya kujiwekea tahadhari mwenyewe.
A-Z MAELEZO YA WEMA
Katika maelezo yake juu ya kilichotokea siku ya tukio, Wema alikuwa na haya ya kusema:
“Nilikuwa natafuta location ya kurekodi muvi yangu kwenye Mgahawa wa Last Drop pale Mwanamboka, nikawa nimepaki nje, nilipotoka nilimkuta mwanamke ndani ya gari nyeupe lililopaki pembeni mwa gari langu.
“Nilikuwa simjui huyo mwanamke ‘so’ nikamchukulia kama mmoja wa haters, (wenye chuki), akaanza kufanya fujo wakati mimi huwa siwezi fujo, nikajitahidi kutoka eneo la tukio na kupiga simu polisi, wakaja kumchukua huyo mwanamke na kwenda Kituo cha Polisi Oysterbay (Kinondoni).
“Kusema kweli mimi sitembei na mwanaume wake wala mume wa mtu, isitoshe yule ni mwanamke ni mtu mzima sana, hawezi kugombana na mimi ‘coz’ kwake najiona mtoto mdogo, akitaka aje na uthibitisho wa kile alichodai.
“Yule mwanamke alisema gari ninalotembelea ni lake. Ukweli gari ni langu kwani hata kadi ninayo ndiyo maana nimelichukua na sasa liko gereji.
“Alinidhalilisha sana ‘so’ siwezi nikaachia hiki kitu kiishe hivihivi kama anavyotaka.
”Kama kweli ningekuwa namchukulia mumewe, sidhani kama ningekuwa nimefikishana naye hapa tulipofika kwa sababu ningeogopa, sasa simwogopi na afanye chochote anachotaka.
“Naomba watu waniache na maisha yangu, nimekaa kimya lakini bado wananifuatafuta.”

SAKATA LIKO POLISI
Kwa mujibu wa data za ndani, sakata hilo lilichukua sura mpya baada ya Wema kumtupa selo Oysterbay mwanamke huyo kwa shitaka la kuharibiwa mali na kutishiwa kupigwa, kuuawa yenye jalada namba OB/RB/4576/2012- TISHIO NA UHARIBIFU WA MALI.
Hata hivyo, mwanamke huyo yuko nje kwa dhamana huku kesi hiyo ikitarajiwa kutinga mahakamani.

WEMA HUYU HAPA TENA, LAITI AGEKUWA ANAKUSANYA KWA KILA CHAPISHO ANGUKUWA MIONGONI MWA MATAJIRI WADOGO HAPA NCHINI ILA MPAKA SASA ANA UTAJIRI WA.......(MTAZAMO TU)

CHANZO; GLOBAL

Posted by Osxarguder • The Creator • on 9:05 AM. Filed under , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for LAITI WEMA AGEKUSANYA KWA KILA TOLEO LEO AGEKUWA MILIONEA HUENDA ILA ANA UTAJIRI WA....

Post a Comment

LETS HOOK UP

.

.
.
slide

SIRI YA MTUNGI PHOTO CAPTION

Recently Commented

ALBUM YA BONGOFILM

SIMULIZI ZILIZOBAMBA KWENYE KURASA ZA KIJAMII

TAKE ONE -HBABA NA FLORA INTERVIEW

2009 Bongofilmdatabase. All Rights Reserved. - Designed by Oscar kwa ushirikiano wa SimplexDesign