RIDHIWANI; SUBTITLE BADO NI UTATA KATIKA FILAMU ZA KITANZANIA
habari, mpya, slide 12:34 PM

Ridhiwani akilishwa keki na Jb huku wasanii wengine wakishuhudia.
Mdau huyo mkubwa wa vijana amewashauri watengenezaji wa filamu kufika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kuwaona Maprofesa na wataalamu wa Lugha kwa ajili ya kuwatafsiria kiingereza katika lugha bora na yenye kuleta maana na si kama ilivyo sasa ambapo wanaharibu lugha za watu.

Riche akisakata Rumba kitaalam.
“Wafuateni wataalam pale chuo kikuu wapo watawasaidia waambieni tusaidieni kama watasema wanataka milioni wapeni hata laki tano kwa kuwaomba ili kuijenga tasnia hiyo ya filamu, pia kuweni wabunifu zaidi tuone kitu tofauti na si kitu kile kile,”anasema Ridhiwan.
.
Sherehe hiyo ilifana sana kwani wasanii hawa nyota pamoja na kuwa mahiri katika uigizaji lakini pia kumbe ni mahiri katika fani ya muziki baada ya kuimba nyimbo na kusakata rumba kwa kiwango cha juu, na kivutio zaidi alikuwa ni Steve Nyerere, Chiki Mchoma rapa nambari moja Bongo movie huku Richie, Mainda, Kupa na JB wakibuka kwa kumwaga viuno vya kufa mtu ilipendeza.
on Mar. 19th, 2012 by