''I THINK I HATE MY WIFE V/s IF I LOVE MY WIFE''




Na. Mwandishi wetu
Miezi kadhaa ilyopita katika kiwanda cha filamu hapa nchini kuliibuka janga moja ambalo kamwe wadau hatuwezi kulisahau la Watayarishaji na waigizaji filamu hii  kushutumiana na kutishiana vikali dhidi yao wenyewe juu ya kuibiana mawazo (idea) kama si kazi nzima kabisa, hali kadhalika suala hilo halikuwa kwa upande wa watayarishaji na wa chezaji tu bali hata kwa wasanii wachanga alimaarufu  huitwa  chipukizi ama undergrounds kwa lugha ya kigeni nao waibiwa na kudhulumiwa kazi zao ,  baada ya muda mfupi kidogo janga hilo likatoweka taratibu  kama wingu nene la mvua kubwa zenye kuhamisha wakazi wa maeneo fulani hapa mjini Dar es salaam bila ya hata kuambiwa na mtu , jamani!!  jamani! wanaoishi mabondeni tunawaomba muhame makazi yenu kwa hofu ya kukumbwa na mafuriko  kama waambiwavyo utawala...

kutodumu kwa janga hili katika tasnia ni kutokana ukweli wa uibiwaji kazi na mawazo ya mtu ni kutokana na mazingira ya uibiwaji kazi zenyewe na hata wengine kutumia nafasi kama hizo kumchafulia mwenzake, kutaka kurejea tena kwenye chati za juu ama kutokea kabisa kwa hawa undergrounds wanao chipukizi kutumia fursa ya namna hii ya kudai wameibiwa kazi zao na wasanii ambao wamekwishatoka na kuwa na majina makubwa tayari na yote hii imefanikiwa kutokea na kutawala vinywani na masikioni mwa wapenzi wa tasnia hii ya maigizo kutokana na upatikanaji wa  mianya mingi kwenye vyombo vingi vya habari kushadadia habari na taarifa za namna hii kwani siku hizi mambo ya husianayo na wadau wa tasnia hii kuwa ndo bidhaa sindikizi katika vyambo vyao vya habari vikiwemo magazeti, redio na televisheni

Janga lingine la filamu hizi kufanana na kuwianamajina likaibuka .nalo  likazua jambo kwenye magazeti na mitandao ya kijamii pia.

Sehemu ya kazi hizo zilizo endesha vipindi vya redio, televisheni na kuuzia magazeti ni kazi zifuatazo ni hizi za wakongwe katika tasnia hii kama marehemu Kanumba, na Ray. kazi zao za THIS IS IT! na  WHAT IS IT? kufanana na kazi za huko hollywood, suala hili nalo likapepea taratibu mpaka kutokomea sasa.


TIZAMA HIZI HAPA CHINI 


V/s

WHAT IS IT?  ya Ray kigosi ambayo hatujafanikiwa kuipata picha ya kasha lake ila ilifanana  na hii hapa chini



Wingu la namna hii tunakutanalo tena kwenye filamu ya Simon Mwapagata kuwa kama ina utata ndani yake juu ya jina la filamu yake  ya'' I THINK I HATE MY WIFE''  na hii ya ''I THINK I LOVE MY WIFE'' ya Chris Rock kitu ambacho Bongo Film Database kwa kushirikiana na mmoja ya wadau wa ukurasa huu bwana Markus tulijiuliza maswali sana na kujua hoja hii, Je! bwana Simon alipata wapi wazo la kuanda filamu yake hiyo ya '' I THINK I HATE MY WIFE'' . jibu la hoja yetu ya msingi kabisa  ilikuwa ni la Bwana Simon kuandaa filamu yake  mara baada ya kuiona hii  kazi ya Chris Rock ya '' ITHINK I LOVE  MY WIFE'' ?! jawabu hili halikamilika mpaka pale Bwana Simon atakapo sibitisha upande wowote kwenye hili.

Dawati letu wahariri likafanya jitihanda zakumtafuta Bwana Simon  na zoezi hilo zikazaa matunda mazuri na tukafanikiwa kumpata Simon ,  ndani ya muda mfupi sana  na tukafanya naye mahojiano  kwa takribani dakika tano na sekunde kumi na saba hivi kuhusiana na hili suala la jina ya kazi yake kuwa  hivyo kitu ambacho mara moja tu kwa mtu  akiyeyaona majina haya  kwenye kasha za kazi hizi ni lazima atakuwa na swali la kujiuliza kama sio kuuliza mtu wa pembeni yake.... Je! Simon aliandika filamu hii kuijibu filamu hii ya chris Rock iliyotoka mwaka 2007? na kutoa yake mwaka jana tu 2011?

(Mtayarisha/Mwigizaji)

Bwana  Simon aliweka bayana suala hili na kusema, kipindi anaitengeneza filamu hii ya kwake hakuwahi kufikiria kama kunaweza kuwa kuna jina kama hilo katika ulimwengu huu wa sinema na kukiri  kuwa majina ya hizi filamu mara nyingi hufanana sana na hata mawazo pia hufanana kama sio kugongana  wakati mwingine ila kwa kazi hii yake ya '' I THINK I HATE MY WIFE'' haifanani hata sehemu na hiyo filamu ya Chris Rock ya '' I THINK I LOVE MY WIFE'' na kusema kazi za kitanzania hupewa majina ya kiingereza kutia ladha nzuri tu pale alipoulizwa kwanini aliamua kuita jina hilo?

PICHA YA KASHA LA ''I THINK I HATE MY WIFE'' NA MUHTASARI WAKE HUU HAPA KWA MUJIBU WA BWANA SIMON TULIVYOZUNGUMZA NAYE KWA NJIA YA SIMU



''I THINK I HATE MY WIFE''

''Biashara na mafanikio yangu yalikuwa kikwazo kikubwa sana  kwa marafiki zangu pale ofisini, kunivuta na kuniweka chini  halikuwa jambo jepesi hata kidogo kwa upande wao hata kwa nguvu za pesa wala namna yeyote ile.  ila mtego wa penzi  la mwanamke huyu  tu walifanikiwa kuniweka mahala walipohitaji niwe kwani kila mwanaume ana udhaifu wake tena utokomea na kupotelea humo kwenye upungufu wake kwa mwanamke yeyote yule atakapopaliwa  mate kila amwonapo na kuzungumza naye jambo la aina yeyote...

Kudhalilishwa na mke wangu mbele ya watumishi wenzangu ilikuwa ni kitu cha kawaida sasa .kumwacha sikuweza japo nilihisi kumchukia kwa vitendo vyake na utumwa wa penzi lake  ulikuwa ndo mfumo wa maisha yangu sasa.


''I THINK I LOVE MY WIFE''


A married man who daydreams about being with other women finds his will and morals tested after he's visited by the ex-mistress of his old friend.
Director:
Chris Rock
Writers:
Chris Rock (screenplay), Louis C.K. (screenplay),and 1 more credit »
Stars:
 Chris Rock, Kerry Washington and Gina Torres

Shukrani nyingi zimfikie Bwana Markus Mpangala (mdau)
R.I.P Steven
Asante!

>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>