JE? KIBONGO BONGO Make-up NI KUUVAA UHUSIKA KATIKA MAZINGIRA YA KITANZANAI?
habari, slide, udaku 11:36 AM
Make-up kwa ujumla tunaweza kusema na kumaanisha kitu chochote kitachotumiwa usoni au kwenye ngozi ya mwigizaji kufanikisha mwonekano unaokusudiwa. na kwa kufupi kabisa twawezasema waigizaji wote hutumia mapambo[make-up] pale awapo mbele ya akamera kwa dhumini la kupiga picha, kusudi lingine mbai na kutaka kuwa mwonekano fulani bali hutumia kuweza kujing'arisha wao na hata picha wapigazo. wakati mwingine make-up utumika kutengeneza sifa za mwonekano wa mwigizaji kwa mfano pua ya bandia iliyovaliwa na Nicole Kidman kwenye filamu ya The Hour kama Virginia Woolf kama unavyona hapo kwenye hizo picha kwa juu utamwona Nicole katika mwonekano wake wa kawaida [picha namba 1] na picha namba 2 ni Nicole katika filamu ya The Hour akiwa amevaa uhusika wa Virginia Woolf yaani ule utofati wa mwonekano wake upo tofauti sana anavyokuwa katika maisha yake yale ya kawaida .
Make-up ndiyo vitu sahihi kabisa kutengenezea/kubumba majeraha,vidonda,na hata kumbadirisha mwigizaji awe anamwonekano wa jitu au kiumbe cha ajabu kifananacho na mwanadamu.
Swali kwa wadau wenzangu wa kitanzania ni vipi tunazitumia hizi make-up kwenye utengenezaji filamu zetu? au ndiyo utakwepa na kunijibu jibu la kila siku nisilolipenda la ''Eti! msanii mzuri ni yule anayevaa uhusika na kucheza uhusika wake kama anavyotakiwa katika uhalisia wa mazingira ya kitanzania.''