ETI! LULU NI MJAMZITO?
mpya, slide, workshop 1:38 PM
KATIKA KUPITA PITA KWETU MITANDAONI LEO, MMOJA WA WAANDISHI WA UKURASA HUU WA BONGO FILM DATABASE AMEKUTANA NA HABARI HII KWENYE KURASA ZA GAZETI LA AMANI LA TAREHE 26 MWEZI HUU IKISEMA YA KUWA ELIZABETH MICHAEL a.k.a LULU NI MJAZITO KWA SASA, SWALI AMBALO LINA UTATA MKUBWA NDANI YAKE NI JE? UJAUZITO HUO NI WA MAREHEMU AU NI MTU MWINGINE? SOMA HAPO CHINI NAMNA MAKALA HIYO ILIVYOANDIKWA NA Hamrani...
Gumzo lililochukua nafasi Jumatatu iliyopita kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar wakati msanii wa filamu Elizabeth Michael ‘Lulu’ alipopandishwa kizimbani, ni juu ya mwonekano wake ambapo kitumbo kilionekana kujaa na kuwafanya watu wahoji, ni mjamzito?
Akiwa mahakamani hapo, baadhi ya watu waliomuona binti huyo anayekabiliwa na kesi ya kuhusishwa na kifo cha Steven Kanumba, walisikika wakiulizana juu ya alivyonenepa ghafla akiwa gerezani na kuhitimisha kuwa huenda ana ‘kibendi’.
“Ona hipsi zilivyoongezeka ghafla, pia tumbo halidanganyi… inaonekana ndani kuna kitu kwani ni vigumu kwa mtu aliye gerezani kwa tuhuma nzito kama za mauaji kunenepa hivi, huyu si bure, atakuwa na mimba,” alisikika akihoji mmoja wa wanawake waliokuwa mahakamani hapo.
Dalili akiwa Oysterbay Polisi
Mmoja wa marafiki wa karibu wa msanii huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake, aliwahi kumtonya mwandishi wetu kuwa wakati Lulu akiwa lupango katika Kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar, alikuwa akichagua vyakula, kitu ambacho ni cha kawaida kwa mtu mwenye ujauzito.
“Kipindi Lulu yupo pale Oysterbay, nilihisi kitu kama hicho lakini siwezi kukithibitisha, alikuwa akichagua vyakula sana kama walivyo wajawazito,” alisema shosti huyo.
Segerea nako
Ikazidi kudaiwa kuwa hata huko Segerea aliko kwa sasa, staa huyo amekuwa mchaguzi wa vyakula, mazingira yanayowafanya watu wake wa karibu wahisi kuna kitu nyuma ya pazia.
Madai ya ugomvi wake na Kanumba
Huko nyuma, siku chache baada ya kifo cha Kanumba, iliwahi kudaiwa kuwa chanzo cha mgogoro kati ya Lulu na marehemu ni baada ya Kanumba kumtaka atoe ujauzito aliokuwa nao ambapo binti huyo aliweka ngumu na kusababisha hali ya kutoelewana kati yao.
Hata hivyo, licha ya tetesi hizo, bado gazeti hili linaendelea kufanya uchunguzi wake na ukweli utakapojulikana utaanikwa.
chanzo; global publisher.