MJUE VILIVYO BOND BIN SINNAN LEO
habari..., mpya, nyota, slide 12:47 PM
Bond Bin sinnan
[Director,producer,actor,Story writer and Presenter]
Kijana huyu alipatiwa jina la Abdallah Suleiman Bin Sinnan na wazazi wake mara
baada kuzaliwa munamo mwaka 1983 huko kanda ya ziwa kwenye mkoa mmoja maarufa
sana hapa Tanzania kwa kupatika samaki baridi mkoa uitwao mwanza pale hospitari
ya bugando .
Abdallah alianza kujihusisha na mambo ya sanaa mwaka 1999
mpaka sasa anatimiza kama kumi na moja katika tasnia hii ingawa hukuanzia moja
kwa moja kwenye tasnia ya maigizo,
alianza na upande wa uimbaji pale awali. Hakufanikiwa kupata elimu za sanaa
katika shule zitoazo masomo ya husianayo na sanaa yake kwa hapa nchini bali
alifanikiwa kuitafuta elimu hii kwa njia ya mtandao kwa lengo la kujiweka sawa
ukiachilia mbali kipaji chake binafsi.
Abdallah hutumia muda wake waziada kujifunza vitu vya ziada
kuza na kutizama ni changamoto zipi wadau wakubwa katika tasnia zinawakabili
katika ulimwengu huu wa sinema kwa kutizama filamu zao wakiwemo watayarishaji
na waongozaji wa kazi za ndani na nje ya Tanzania.
Vitu ningine anavyovipenda ni kuimba na kutangaza pia kitu
ambavyo anavihusudu kwa sana,kipindi kile cha nyuma alikutana na wakati mgumu
sana kuingia kwenye hii tasnia kutokana na kuwepo na uelewa mdogo wa watu na
mambo haya ya maigizo tena ukizingatia ilikuwa ni huko mkoani hivyo
alikabiliana na changamoto hiyo na ilikuwa ikimweka kwenye wakati mgumu sana
kwa kila aliyemweleza ya kuwa yeye ana uwezo wakuigiza alionekana kama
anaongopa.
Hali hiyo ilikuja kubadirika kabisa mara tu alipopata nafasi
ya kutokeza na kuonekana kwenye luninga na kufanya vizuri kutokana na yeye kuwa
na uzoefu na haya mambo ya upigaji tangu akiwa mdogo sana hivyo ule muwashasha
haukumsumbua sana na hata kujiona mbele ya wenzake ingawa yeye anasema umaarufu
husumbua sana kwa mtu aliyeupata bila kujipanga na hatimaye wana kuwa juu kasha
shuka mara moja tofauti na yeye kwani humwomba
sana Mungu na amejaliwa kupata hata washauri wazuri kutoka kwa watu
wanaomzunguka akiwemo mchumba wake.
Kutoka na tasnia hii hapa nchini Tanzania kuwa ile ya
kaka,rafiki katoka na mimi atanisaidia name kwenye upande huu ya tasnia ni
wengi sana ambao amefanikiwa kushirikiana nao katika kazi tofauti tofauti nao
kurudi kumshukuru kwa msaada na mchango aliouchangia kama yeye na hata wengine
kuthubutu kumtizama kama mfano wao[role model] na kwa upande wake watu ambao
huwatizama ni Jacob Steven [Jb] kwa hapa nyumbani, Amir Khan na Mel Gibson toka huko marekani
kutokana na kujituma kwao katika kazi.
Pamoja na kuwa anajiamini kiasi chote hicho cha kuweza kucheza
nafasi tofauti tofauti kwenye filamu aliwahi kushidwa kufikia kiwango
kilichohitajika na mwongozaji wa tamthilia ya Unfaithfull ambapo aliongozwa
acheze kama muhudumu wa bar.siku hiyo hataweza kuisahau maishani mwake kwani
alishindwa mbele ya waongizaji wakubwa toka nje ya nchii hii ya Tanzania ijapokuwa
alijifunza mengi sana kutokana kushindwa kwake huko.
Abdallah amefanya kazi kadhaa mpaka sasa ila kazi ambayo
alimelipwa vizuri naye kuona anatambuliwa vyema kwa mchango wake kwenye
kuifaniksha kazi hiyo ni filamu ya Lost Souls iliyotoka wiki kadhaa zilizopita.
Na mtizamo wa tasnia hii hapa Tanzania kwa upande wa abdallah alikuwa na haya
ya kusema; ‘‘Imepanda sana kuanzia
Kiubora mpaka mapato hilo liko wazi ingawa bado kila kitu hakilingani na hadhi
yake, ila baadhi ya wasanii hawalipwi vyema kama filamu zao zinavyowafaidisha wasambazaji hivyo bado kuna tatizo
hilo ambalo ni kubwa na lisipoangaliwa tutarudi tulikotoka’’. Na kwa washaiki wangu wote, jamani mie kijana wenu sina cha kusema sana
ila nawaomba muendelee kunisapot na kuniunga mkono pia msiache kunikosoa
ninapokosea na kunishauri ili niendelee kusonga mbele,
Mungu awabariki sana
. Mwabeja sanaa ' maana yake asanteni sanaan kwa lugha ya mama yangu kisukuma
hahahaa..
TUMA BIOGRAPH YAKO LEO KUPITIA MAIL YETU NAWE TUKUANDALIE KITU CHA
NAMNA HII
Mail; bongofilm@hotmail.com
SHUKRANI NYINGI KWA ABDALLAH a.k.a Bond Bin Sinnan