NDOA YANGU...NDOA YANGU



Kazi ya mwisho kuchezwa na kutayarishwa na marehemu Steven Charles Kanumba ambayo ilikuwa tayari kuigia sokoni mapema mwezi wa nne mara baada kuifanyia matangazo yakutosha kwenye  magazeti,redio na kubandika poster zake  mitaani  ila suala hilo lakuitoa filamu hii ikashindikana kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wasambazaji [Steps] za kupokea taarifa za kumpoteza mtayarisha mkuu wa filamu hii usiku wa kuamkia tarehe saba mwezi wa nne sasa  ipo tayari kwenye orodha ya filamu zitakazo toka hivi karibuni... kaa mkao wa kuburudika na kuelimika sasa....

 Filamu;
 Ndoa Yangu

Mtayarishaji.
Steven Kanumba

 Director
Steven Kanumba.

Star Cast;
Steven Kanumba.
Jackline Wolper
Patcho Mwamba


 ------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

 Leo wino wa  Bongo film Database unamwagika kwenye alama za angalizo[Film Censorship] zitoazo onyo juu ya umri wa wanaopaswa kuangalia filamu kwa maana ya  kwamba mambo yanayozungumziwa ndani yake ni mahususi kwa rika fulani kwa  mfano PG kwa rika lolote wanaweza tizama uhususani watoto zaidi kutokana na mfumo wa hadithi yenyewe na hata mazingira iliyochezewa daima huwa sawiya na yale mazingira yao ya kila siku yanayowapa furaha siku zote. ,PG 13 ni mahususi kwa watoto kuanzia miaka kumi na tatu na kushuka chini kwa kiasi fulani, PG (15-16)  ni mahusi kwa watu wenye umri huo tu. Hii inayoonesha kuwa imewekewa nembo ya  PG 18+ ni mahususi kwa watu wenye umri wa miaka kumi na nane na zaidi tu



Alama hizi zilitambulishwa kwenye ulimwengu huu wa sinema mapema mwa mwaka 1907 huko nchini Marekani kwenye moja ya majimbo yake lijulikanalo kama Chicago mara baada ya bodi maalumu ya ukaguzi wa mambo ya maadili ndani ya jamii kuingiwa na hofu juu ya maadili ya jamii yao kumomonyoka kwa sinema zilizotengezwa nchini humo kuwa na mambo ambayo moja kwa moja yatapelekea kumomonyoa madili iliyokuwa inaoneshwa kwenye majumba ya sinema na  munamo mwaka 1908 nchini humo humo mliki wa jumba moja alitiwa nguvuni mara baada kuonesha filamu ilyokuwa na vipande visivyofaa kuoneshwa kwa watu waliochini miaka kumi na nane na  kumtia nguvuni kwa mliki wa ukumbi huo ilikuwa kama mfano na fundisho lenye onyo kali kwa wale wote watakao kiuka agizo hilo tena.

jamani kwa hapa Tanzania kwani alama hizi zina umuhimu kweli? kwani mpaka leo hii hakuna hatua zozote zilizochukuli dhidi ya watayarishaji filamu juu ya kazi zao zilizokuwa vipande visivyostahili kuoneshwa kwa rika fulani na fualani badala yake utawasikia wakilalamika siku zote ya kuwa wasanii wapotosha maadili...watayarishsji ukizungumza nao utawasikia wakihoji na kusema kwani kuna umaana gani hasa kuwekwa alama hizi kwenye kasha la filamu? ukuitaza bodi yenyewe husika haiko makini... ila  swali hili jibu lake nimekwisha taainaisha hapo juu ila  pamoja na umaana wa alama hizo kuwa ni muhimu sana zingatiwe na watayarishaji kwa jamii yetu kwe utendaji wao wakazi kwani alama hizi  sio ngeni kabisa kwa watayarishaji filamu wetu ila  bado hazipewi nafasi kabisa sasa sijui ni kutozingatia maadili ya taifa letu kwa ujumla wake au ndiyo  shetani wa pesa  anyewavuta wakati wakijitambua? ndugu zetu tuangalie tunakotoka, tulopo na tunakoelekea kwa jamii hiyo inayohalibika ndiyo jamii hiyo hiyo watakuja ishi watoto wenu na wa wenzenu.

Juhudi za kuwatafuta wazalishaji filamu hapa nchini  tukazifanya na kuzungumza nao kwa njia tofauti tofati na mmoja wao alikuwa na haya ya kusema;


Mtayarishaji;
                         -- ''Hapa Tz tatizo ni Bodi ya ukaguzi filamu nchini [TFCB] kwani  wao ndo hasa wanaotakiwa ku-rate movies, lakini ninachokijua mimi ni kwamba hawana muda wa kufanya hiyo kazi na labda hawaijui kabisa. mfano mimi ni mzuri sana kwenye filamu za kiutu uzima lakini hata unawapelekee script hawaipitii kwa umakini basi tu mtu unajiandikia unavyotaka.'' 



Mfano filamu ya ndoa yangu ina alama kwenye kasha lake ikianisha ama kutahadhalisha watizamaji yakuwa ina mambo ambayo kimsingi yanafaa kutizamwa na watu wenye rika la miaka kuanzia kumi na nane na kuendelea tu ila kutokana na mazingira ya tasnia yetu hii ya watu wanao tayarisha filamu kutozingatia hata kidogo suala hili na kusahau wao ndiyo wanachangia kudumisha mila na tamaduni zetu kwa kiasi kikubwa na badala yake ndivyo tuanavyoona sasa au tuwageukie tena na kuwauliza watu wa serikalini kupitia wizara yake inayosimamia mambo ya sanaa hapa nchini? hapana! sisi kupitia ukurasa huu tunanuiya kutoa elimu madhubuti kwa jamii juu ya hili suala na kwa kuanzia tuanpenda kuanza na hii filamu ya marehemu Steven Kanumba itakayoingia sokoni hivi karibu, jamani watanzania wenzetu uhususani wazazi tunapenda kuwaasa juu ya hili...chonde chonde tuzitizame filamu hizi kwanza ndipo tuwaruhusu nayo wazitizame sasa kwani filamu za sasa zinafundisha sana hivyo tusiwanyime elimu hii kupitia filamu.






Posted by bongofilmdatabase on 9:24 PM. Filed under , , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for NDOA YANGU...NDOA YANGU

Post a Comment

LETS HOOK UP

.

.
.
slide

SIRI YA MTUNGI PHOTO CAPTION


Recently Commented

ALBUM YA BONGOFILM

SIMULIZI ZILIZOBAMBA KWENYE KURASA ZA KIJAMII

TAKE ONE -HBABA NA FLORA INTERVIEW

2009 Bongofilmdatabase. All Rights Reserved. - Designed by Oscar kwa ushirikiano wa SimplexDesign