WASANI WA KUBWA MTAONEKANA VITUKO MPAKA LINI?


Hivi ni kwanini tunashindwa kuwa serious na films zetu kwa kuiga uzungu usiokuwa na maana na kuonekana vituko huko huko kwa wazungu wenyewe! now nilikuwa naangalia film mpya inaitwa Matilda ikiwa imetengenezwa na kuongozwa na Mtitu Game but licha ya film kuwa nzuri ila aliyeharibu film ni Hemed kwa mavazi na muonekano wake usioendana na scenes husika. hili nimeshalizungumzia mpaka basi lakini hatubadiliki wabongo ni kwanini? yaani mtu anaenda ofisini tena kaajiriwa na siyo ofisi yake bt amevaa vipuli, mbaya zaidi amevaa nguo za kwenye sherehe au tafrija eti ndiyo mavazi ya ofisini. nywele hazieleweki kabisa.
Kila Hemed anapoonyeshwa filamu inakosa msisimko kwa kuwa mavazi yake na muonekano haviakisi uhalisia hata kidogo. Sio Hemed tu mfano mwingine mzuri ni Ray karibia films zake zote anaharibu filamu kwa kung'ang'ania kuvaa vipuli sehemu zisizoruhusu pambo hilo. Hivi kwanini huwa hatuwaulizi watu wanaojua fashion hata kama nguo mtu anakuja nazo mwenyewe location! tutaendelea kuonekana vituko ktk films zetu mpaka lini?. Ni kweli ktk hali halisi mwanaume anaenda ofisini akiwa amevaa vipuli au tunafanya maigizo badala ya films. Director hawezi muongoza actor kama muonekano wake hauendani na character husika so lazima actor apambwe upya au nguo zibadilishwe. Leo ukiambiwa utaje best film directors in Tz jina la Mtitu Game haliwezi kukosekana kwenye top 5 au top 3 so sielewi ni kwanini huwa anaruhusu watu wauze sura in his films badala ya kazi. Generally film iko poa from story to direction.


Mwandishi: Trim Saleem 











Chanzo:Facebook

Posted by bongofilmdatabase on 5:52 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for WASANI WA KUBWA MTAONEKANA VITUKO MPAKA LINI?

Post a Comment

LETS HOOK UP

.

.
.
slide

SIRI YA MTUNGI PHOTO CAPTION


Recently Commented

ALBUM YA BONGOFILM

SIMULIZI ZILIZOBAMBA KWENYE KURASA ZA KIJAMII

TAKE ONE -HBABA NA FLORA INTERVIEW

2009 Bongofilmdatabase. All Rights Reserved. - Designed by Oscar kwa ushirikiano wa SimplexDesign