DUME JEURI NI MKOMBOZI NA IMEIBUA HISIA CHANYA KWA WALIOPUUZWA


Uwezo wa msanii huzihilika pale apewapo nafasi bila kutiliwa shaka nae hujisikia ni msanii muhimu kwenye kuikamilisha filamu mpaka inakwenda sokoni, jambo hili limeelezwa na mwigizaji na mtayarishaji filamu wa siku nyingi Bw. Chiki Mchoma ama kwa jina lake maarufu la Teacher kutoka kwenye kisima na kiini  cha wasanii waliyoijenga tasnia hii ya maigizo hapa nchini, Kaole Sanaa Group chenye makazi yake hapo kigogo sambusa na kambi yake kuu ilyopo hapo Magomeni mkwajuni.

Bw. Chiki aliendelea kuzungumza na kuweka bayana magumu alioyapitia katika utayarishaji filamu yake hii ya kwanza  ya DUME jeuri kwa kusema; Uwezo wa wasanii niliowatumia himu kwenye filamu hii ulikuwa wa kati hivyo nikalazimika kuingia nao kambi kwa muda wa taklibani miezi miwili hivi na kuwapika vilivyo vijana hawa kwani nilikuwa nina imani yakuwa watafanya vile nilivyokuwa nategemea tangu awali.

Mazungumzo kati ya Bw. Chiki na mhariri wetu kwenye ukurasa huu wa Bongo film Database hayakuishia hapo, mwandishi akamtaka afunguke kidogo. Kwanini filamu zetu zina sura zilezile kila siku?. Bw. Chiki alikuwa na haya juu ya swali hilo; kiukweli namshukuru Mungu kazi imekubalika kwa kila aliyeiona hakika imeondoa dhana iliyojengeka kuwa filamu ni lazima wacheze kina fulani na 

kwenye makava wakae wao..Dume Jeuri ni mkombozi halisi wa hisia Chanya za wasanii waliopuuzwa.

Asante Bw.Chiki Mchoma na Mungu abariki kazi ya mikono yako.
CHIKI: ''ISIPOKUPA RAHA IRUDISHE KWANGU FASTA NITAKURUDISHIA MKWANJA WAKO!!''

Posted by bongofilmdatabase on 12:03 PM. Filed under , , , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for DUME JEURI NI MKOMBOZI NA IMEIBUA HISIA CHANYA KWA WALIOPUUZWA

Post a Comment

LETS HOOK UP

.

.
.
slide

SIRI YA MTUNGI PHOTO CAPTION


Recently Commented

ALBUM YA BONGOFILM

SIMULIZI ZILIZOBAMBA KWENYE KURASA ZA KIJAMII

TAKE ONE -HBABA NA FLORA INTERVIEW

2009 Bongofilmdatabase. All Rights Reserved. - Designed by Oscar kwa ushirikiano wa SimplexDesign