TIMAMU AFRICA MEDIA WASIMAMIA WASANII KITAIFA NA KIMATAIFA
habari, habari..., jifunze, mitandao, slide 11:28 AM
Timamu African Media, watayarishaji wa filamu ya Mdundiko,Kisate na nyingine zilizofanya na zinaendelea kufanya vizuri sokoni kwasasa. Kampuni hii inayoundwa na vijana wadogo tu wenye ndoto yakuona maisha ya sanaa ya maigizo yanakuwa yenye mafanikio hapa nchini na hata siku moja wasanii wakitanzania wanakabidhia bendera ya taifa letu kwenda kuipeperusha vilivyo kama wanamichezo wengine wanaofanya vizuri.
Timamu Casting Agency (TCA), Ndiyo kitu kipya kutoka kwenye kampuni hii ya utayarishaji filamu hapa nchini, usahili wa awali ulifanyika pale Atriums Hotel iliyopo sinza africasana, ilikuwa tarehe 21
mwezi wa sita mwaka huu, judges walikuwa ni Cloud 112, Dokii, Julieth
samson Kemy, Costantino Solo (Mkufunzi Chuo Kikuu cha mlimani).
Usahili kwa awamu nyingine utatangazwa siku si nyingi ili kuwapa nafasi zaidi wasanii wenye vipaji kuigia kwenye benki hii ya Timamu kwa lengo la kupata fursa ya vipaji vyao kunadiwa kitaifa na hata kimataifa.
Mtangazi akimwoji mmoja wasanii waliyofika kwenye usahili
kwa mawasiliano na taarifa zaidi waweza kuwasiliana na mkurugenzi mkuu Bw. Timoth Conrad kupitia kurasa wa facebook wa Timamu Africa Media
Asante