WIZI WA KAZI ZA WASANII MBIONI KUPATIWA DAWA
kinyemi, mpya, slide 12:38 PM
Huenda kilio cha wasanii
juu ya wizi wa kazi zao kikapungua kama si kufikia kikomo iwapo wasanii
wataamka na kushirikiana na kampuni ya Global Standard One (GS1) ambayo imekuja
na mfumo wa kimataifa wa kutambua na kudhibiti kazi za Sanaa.
Akizungumza wiki hii kwenye
Jukwaa la Sanaa la Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Kaimu Mkurugenzi wa kampuni
hiyo Fatma Kange alisema kuwa, mfumo huo wa kuziwekea alama ya utambuzi ya
kimataifa (barcode) kazi za wasanii utasaidia kudhibiti uharamia kwenye sekta
ya sanaa na kusaidia upatikanaji wa takwimu sahihi.
“Mfumo huu ni wa kimataifa,
umekuwa ukitumika duniani kote miaka 38 iliyopita, hapa kwetu ni mpya kabisa.
Ni mfumo wa kutambua bidhaa halali kwa kuziwekea alama maalum (barcode) ambayo
itazifanya zitambuliwe kimataifa na kutokughushiwa” alisema Bi. Kange.
Aliongeza kuwa, mfumo huo
unalenga kurasimisha sekta ya Sanaa kwa kuwafanya wasanii kwanza kujisajili na
baadaye kazi zao kuwekewa alama maalum ambapo sasa watajua idadi halisi ya nakala
(bidhaa za sanaa) walizozalisha, fedha walizoingiza na zaidi kutazuia kazi zao
kuuzwa hovyo mitaani pasipokufuata taratibu.
“Lengo ni kazi za wasanii
kutambuliwa kimataifa, kuuzwa kwenye maduka makubwa na kupewa thamani halisi.
Wenzetu katika nchi zilizoendelea wako mbali katika hili, kazi zao zinauzwa
kwenye art stores tu (maduka maalum ya kazi za Sanaa)” alisisitiza Kange.
Akieleza jinsi Wasanii
watakavyojiunga, Bi. Kange alisema kuwa, wako kwenye mikakati ya kuwaelimisha
Wasanii lakini akasisitiza kuwa, mfumo huo huendeshwa kwa wasanii wenyewe
kuridhia na baadaye kazi zao kuwekewa alama hiyo ambapo hukatwa kiwango kidogo
sana cha fedha baada ya kukubaliana na wasanii wote.
Kwa upande wake Katibu
Mtendaji wa BASATA, Ghonche Materego alisema kuwa, kwa muda mrefu sekta ya
Sanaa imekuwa ikichukuliwa kama ya burudani tu kwa hiyo muda umefika wa
watanzania kuichukulia Sanaa kama biashara na kuipa thamani halisi.
“Kwa sasa Sanaa
imekubalika, ule wakati wa kuiona kama burudani tu umepita. Hatuna ujanja
lazima tuirasimishe sekta ya Sanaa” alisisitiza.
Aliwaahidi Wasanii kupitia
mashirikisho na vyama vyao kuwa, kutakuwa na vikao vya mara kwa mara na kampuni
hii ili kuona ni kwa kiwango gani suala la udhibiti na utambuzi wa kazi zao
kupitia nembo hii linaweza kutekelezwa.
Caption.
1.
Bi. Fatma Kange akiongea na wadau wa Sanaa
kuhusu mfumo maalum wa kimataifa wa utambuzi na udhibiti wa bidhaa mbalimbali
wakati akiwasilisha mada kwenye Jukwaa la Sanaa la BASATA mapema wiki hii.
Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti, Mafunzo na Habari, BASATA Godfrey
Lebejo na Katibu Mtendaji wa BASATA, Ghonche Materego.
2.
Katibu Mtendaji wa BASATA, Bw. Materego
akisisitiza jambo wakati akiongea na wadau wa Sanaa kwenye Jukwaa la Sanaa la
BASATA wiki hii. Alieleza kuwa, ni wakati sasa wa kuirasimisha sekta ya Sanaa.
3.
Mtendaji kutoka Kampuni ya Global Standard
One (GS1), Andrew Karumuna akionesha moja ya kazi ya Msanii Judith Wambura
(Lady Jay Dee) iliyowekewa alama maalum ya kimataifa ya utambuzi na udhibiti wa
bidhaa kwenye Jukwaa la Sanaa wiki hii.Lady Jay Dee ni msanii pekee ambaye
amekwishaingia na kuanza kunufaika na mfumo huu.
4.
Mdau na mkereketwa wa Sanaa na Jukwaa la
Sanaa, Francis Kaswahili akiuliza na kuchangia mada kuhusu mfumo huo wa
utambuzi na udhibiti wa bidhaa mbalimbali zikiwemo za Sanaa.
5.
Mdau huyu alipongeza ujio wa mfumo huu
lakini akataka Wasanii wahamasishwe kuingia katika mfumo ili kudhibiti
uharamia.
6.
Sehemu ya Wadau wa Jukwa
Na
Mwandishi Wetu
Asante!
(c) Bongo film data base