TAFF YAWATAKA WASANII WOTE WACHAFU KATIKA TASNIA KUJITOA SUMU YA UOZO NA SI KUJIVUA GAMBA TU KAMA....

Taff  kupitia mkutano wake wa hadhara na wadau pamoja na wasanii uliyofanyanyika t ng'aka na kuonyesha meno na mamlaka waliyokabidhiwa na vyombo vya sheria nchini chini ya mwanvuri wa basata na wizara kwa ujumla dhidi ya mambo ya msingi na yasiyokuwa na msingi kwa jamii toka kwa vioo vya jamii vipendwavyo kwa sasa mitaani na uswailini kwetu wasani waigizaji hususani upande wa tasnia ya filamu kuwa na maadili ya kugeza toka mataifa ya mbali yaliyo na utamaduni tofauti kabisa na tuliyokuwanao kwetu tanzania na afrika kwa ujumla...  

Hoja zilizo zungumziwa zilikuwa nzuri kwa ujumla kwa malengo mazuri kwa kizazi kinachokuja hapo badae  kwenye ulimwengu huu wa sanaa na hata kwa wadau watizamao kazi za wasanii kwani bila ya wadau hakuna mtu kwenye tasnia hii wakuzungumza jambo na kuonekana mtu mbele za watu. 

1.usimamzi wa sheria juu ya namna ya utengenezaji filmu zilizokuwa na maadili.
2.kusimamia usambazaji wa kazi za wasanii ipaswavyo kwa manufaa ya mazuri kwao na kwa wa wengine wahusika katika tasnia.
3.kuenea na kusamba kwa shirikisho la filamu mikoa ya jirani kuanzia morogoro,tanga dodoma mwanza na hatimaye nchi nzima.
4.kuhakisha filamu vinakuwa na viwango vyenye ubora maana ya kwamba zinawekewa ngazi(grade)  kuonyesha ni kwa maana ya mgawanyo wa filamu kimakundi ya umri unaotakiwa kutizama filamu hizo.
5.kutangaza filamu katika magazeti ya serikari..

Upande wa pili wa shilingi wa hoja zilizotolewa kwenye mkutano ule hazikukubali zenyewe ziwe chini tu,mara tu zilipo anzwa kutajwa na mtoa maada ama hotuba kwenye mkutano ambaye alikuwa ni rais wa shirikisho la filamu tanzania(TAFF) bwana Simon Mwakifamba, ziliweza kuuamsha umati wa watu waliyokuwa kwenye viwanja vile hususani wasanii  wale yaliwagusa zaidi kwa yaliyotajwa mfano jackiline wolper aunt ezekiel na wengine wengi ambao majina haikutambulika mara moja ..

1.kuvunjwa kwa club maarufu ya bongo movie club ambayo imekuwa ikitembelea sehemu mbali mbali muhimu kama bungeni a.k.a mjengoni na   kucheza  mechi kadha wa kadha na wadau tofauti tofauti hapa nchini na kujipatia pesa nzuri za kutosha na kuongeza wadau pia ambacho kimeonekana kiko kinyume na katiba za taff . club hiyo ilianzishwa kutoka na janga la mabomu ya gongo la mboto kuwa changia msaada wahanga wa mabomu yale.
2.kutengeneza filamu mbovu ambazo zilibatizwa jina la BOX MOVIES maana ya kwamba content zake kwa upande wa location ni hotelini ,mapokezi, ofisini, vyumbani,sitting room,magari ya kifahari na kuvaa vimini wadada wa ofisini tu.
3.filamu kuchochea mambo ya siyofaa kuhamasisha anasa na mmonyoko wa maadili katika jamii zetu kama filamu ya SHOGA.
4.watu kuutaka usuper star kurahisisha maisha yao kwenye upande wa starehe tu husani kwa wa dada na vijana wanao chipukia pia.
5.wadada kujiuza kupitia magazeti hasa hale ya udaku kama kiu,ijumaa,risasi na mengi mwengineyo tunayoyafahamu pia...
KIUKWELI MAMBO YALIKUWA NI MENGI SANA YALIYO WEKWA BAYANA KWA WADAU NA WASANII PALE KWENYE MKUTANO,TUTAENDELEA KUJUZANA NA KUHABARISHANA YOTE HAYA KWENYE MFUMO WA PICHA NA VIDEO CLIP ZILIZOPO STUDIO HUMU HUMU...
karibuni

Posted by Bongo Film Data Base on 1:05 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for TAFF YAWATAKA WASANII WOTE WACHAFU KATIKA TASNIA KUJITOA SUMU YA UOZO NA SI KUJIVUA GAMBA TU KAMA....

Post a Comment

LETS HOOK UP

.

.
.
slide

SIRI YA MTUNGI PHOTO CAPTION

Recently Commented

ALBUM YA BONGOFILM

SIMULIZI ZILIZOBAMBA KWENYE KURASA ZA KIJAMII

TAKE ONE -HBABA NA FLORA INTERVIEW

2009 Bongofilmdatabase. All Rights Reserved. - Designed by Oscar kwa ushirikiano wa SimplexDesign