OMARY CLAYTON MWONGOZAJI NA MWANDISHI WA FILAMU NDANI YA UMRI MDOGO HAPA BONGO HUYU HAPA TENA

Omary clayton,kijana mwenye umri mdogo wa taklibani miaka kumi na tisa(19) sasa na kwa majaliwa yake Mwenyezi Mungu atatimiza miaka ishilini(20) tarehe nane(8) mwezi wa kumi na mbili(12) mwaka huu, mkazi wa eneo ya Magomeni jijini Dar es salaam.

 Omary Clayton, alihuzulia masomo yake huko Tanga na badae  kujihusisha na sanaa kwa muda mrefu sasa alianza tangu alipokuwa mdogo ana miaka kumi na nne mwaka 2005. akajiunga kwenye kikundi cha maigizo miaka hiyo ya 2005 pia na kucheza michezo ya runinga kadhaa hapo iliyorushwa kwenye vituo vya television kama ITV kupitia kundi hilo hilo moja lijulikanalo kwa jina la kundi maarufu sana hapo Dar es salaam na Tanzania nzima kwa ujumla ''KAOLE SANAA GROUP'' lenye makao makuu  hapo Magomeni Mikumi.
 
Omary Clayton, baada ya kuwa karibu sana na makini zaidi na mchakato mzima wa utayalishaji na uzalishaji filamu kwa miaka kadhaa akaijikuta tasnia inamvuta kwa karibu pia na kumwekea mazingira mazuri na kumwandaa Omary kuwa mchezaji mzuri ,mwandishi mzuri wa hadithi na miswada ya filamu mpaka sasa.na ndiyo kazi yake apendayo kwa sasa ndani ya kampuni ya TIMAMU EFFECTS. hupenda kazi yake zaidi kwani muda mwingi hujawa na kui kubwa zaidi ya kufanya vizuri kila siku hasa kajiwekea malengo ya kuongeza bidii kila afanyapo kazi mpya yenye ubora na mvuto zaidi ya kazi iliyopita..  
 
Omary Clayton kazi yake ya mwisho ilikuwa ni HEKIMA  ,filamu ambayo ilikuwa inasisimua sana,
 
STORY; Omary Clayton 
 
DIRECTOR;Omary Clayton,
 
CAST; Hemedi Suleiman ,Sajuki, Wastara, Maida Omary na wengine wengi .
 
Omary sasa amefunguka na kitu kingine, filamu mpya itakayo ingia sokoni mwezi ujao akiwa ameshiriki na kuiongoza mweyewe tena.
 
STORY; Omary Clayton 
 
DIRECTOR;Omary Clayton,
 
CAST; Hemedi Suleiman , Wastara,Omary  Bi mwenda na wengine wengi .
AGE; PG
SYNOPSIS; ugomvi mkubwa unajitokeza kwenye familia unaosababishwa na tamaa ya mali zilizo achwa na mmoja wa familia kupelekea wanaanza kupuliziana na kupeana madawa na ikapelekea familia nzima kuanzia mama,dada ambae ni wastara na shemeji kupata tabu sana mpaka mmoja kuwa mlemavu wa uzezeta wakurogwa na shangazi yao ambaye ndiyo bi Mwenda !!  CHECK IT OUT BY NEXT MONTH...
 
 
 

Posted by Bongo Film Data Base on 5:38 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for OMARY CLAYTON MWONGOZAJI NA MWANDISHI WA FILAMU NDANI YA UMRI MDOGO HAPA BONGO HUYU HAPA TENA

Post a Comment

LETS HOOK UP

.

.
.
slide

SIRI YA MTUNGI PHOTO CAPTION

Recently Commented

ALBUM YA BONGOFILM

SIMULIZI ZILIZOBAMBA KWENYE KURASA ZA KIJAMII

TAKE ONE -HBABA NA FLORA INTERVIEW

2009 Bongofilmdatabase. All Rights Reserved. - Designed by Oscar kwa ushirikiano wa SimplexDesign