K’NAAN KUCHEZA FILAMU YA MAPENZI JIJINI MWANZA HIVI KARIBUNIKama ulifuatilia fainali za Kombe la Dunia mwaka jana nchini Afrika Kusini,bila shaka ulilisikia pia(pengine kwa mara ya kwanza) jina la msanii K’naan,kijana mzaliwa wa nchini Somalia mwenye makazi yake ya kudumu nchini Canada.K’naan alitamba vilivyo na kibao chake cha Waving Flag ambacho ndicho kilikuwa wimbo wa bara zima la Afrika hususani wakati wa fainali hizo zilizofanyikia nchini Afrika Kusini ikiwa ni mara ya kwanza kufanyikia barani Afrika.

Habari nzuri ni kwamba K’naan atakuwa nchini Tanzania hivi karibuni kule jijini Mwanza(Rock City) ambacho atakuja kushiriki katika filamu inayoitwa The Catastrophist ambayo shooting yake utafanyikia jijini Mwanza. K’naan atakuwa sambamba na waigizaji wengine Steve Coogan na Stephen Dorff na itaongozwa na Muingereza Nick Broomfield(huyu jamaa ni mtengeneza documentary maarufu na mojawapo miongoni mwa documentaries alizowahi kutengeneza ni pamoja na ile ya Tupac and Biggie) kupitia kampuni yake ya Lafayette Films.Sambamba na Broomfield,Producers wengine ni Paul Miller wa Escape Pictures na Donall McCusker

Filamu hiyo inatarajiwa kuiongezea nguvu kidogo tasnia ya filamu nchini Tanzania kwani licha ya filamu hiyo kuwa na watu wa kimataifa, filamu hiyo ambayo itakuwa na hadithi fulani ya mapenzi enzi za ukoloni wa Ubelgiji dhidi ya Congo,producers hao wamesema watajaribu kutumia vitu vya hapa hapa Tanzania(mfano magari yatakayotoa picha ya Congo katika miaka ya 1960′s).Kazi kwenu wakazi wa Mwanza.

story by BongoCelebrity.

Posted by Bongo Film Data Base on 12:44 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for K’NAAN KUCHEZA FILAMU YA MAPENZI JIJINI MWANZA HIVI KARIBUNI

Post a Comment

LETS HOOK UP

.

.
.
slide

SIRI YA MTUNGI PHOTO CAPTION

Recently Commented

ALBUM YA BONGOFILM

SIMULIZI ZILIZOBAMBA KWENYE KURASA ZA KIJAMII

TAKE ONE -HBABA NA FLORA INTERVIEW

2009 Bongofilmdatabase. All Rights Reserved. - Designed by Oscar kwa ushirikiano wa SimplexDesign