Awali nikiongea naye alinieleza kuwa hapo mwanzo alikuwa akitumia vifaa kwa kukodi lakini aligundua kuwa ni gharama na aliamua kusafiri kwenda nje kwa ajili ya kununua vifaa vyake kwa ajili ya Production, na baada ya kurudi Swahiba yake alikwenda naye Marekani kwa ajili ya kununua baadhi ya vifaa kwa ajili ya Production.
Mara nyingi Ray amekuwa akianza kufanya jambo na wengine wanafuatia, anastahili kupongezwa yeye ndiye aliyekuwa wa kwanza kabisa kuamini kuwa wasanii wanaweza kuwa watayarishaji na alifanya hivyo japo wapo waliokuwa wakisema hataweza na kurudi kwa Mtitu Game, lakini jamaa alisimama imara.
Msanii huyu baada ya kutoka na filamu ya Johari na kufanya vizuri kupita maelezo alianza harakati zake katika kupigania maslahi yake na hatimaye alitengeneza filamu ya Fake Pastor lakini hakubweteka hapo kwani alikuwa hajafika na aliamua kama yeye kutoa filamu ya Shakira.
Baada ya muda aliingia mkataba na Mtitu kwa filamu kadhaa na alirudi na kuendelea na kuamua kufungua kampuni yake kwa ushirikiano na msanii mwenzake Blandina Chagula hapo ilizaliwa kampuni ya RJ Company ambayo inasumbua Bongo na nchi jirani katika masuala ya filamu.
Najaribu kuongelea sehemu mbalimbali ambazo Ray alipitia ili kukupa uhalali wa kumtangaza kama mwanaharakati na shujaa katika kuleta mabadiliko katika tasnia ya filamu Bongo jamaa ni mpiganaji wa kweli lakini pia mwenye huruma na wasanii wengine kwani sehemu aliyopo ukaribisha na wengine.
Baada ya kampuni ikumbukwe kuwa alitumia nafasi ya ubunifu kuweza kubandika stika katika gari lake la Production na wengine walifuatia, kufanya hivyo kwa kila mtayarishaji anatamani kuwa kama Ray kwa kila kitu lakini kwa upande mwingine inakuwa ngumu.
Hata kuna baadhi ya wasanii wamekuwa wakitumia nguvu ya msanii huyu kujihalalishia mambo Fulani Fulani, kwetu sisi Ray ni Shujaa katika tasnia ya filamu jamaa ana mambo mengi ambayo jamii inatakiwa kuiga kutoka kwake ni mjasiriamali, mpiganaji asiyechoka.
Lakini pia ni mtu mwenye msimamo kwa kile anachoamini jambo ambalo limekuwa ni chachu ya maendeleo yake katika utendaji wa kazi zake za filamu na maisha kwa ujumla.
Mwaka huu tunaanza na uchambuzi huu wa kuwatambua wapiganaji wanaoleta changamoto katika filamu Bongo, kwani yeye ndio alikuwa mtu wa kwanza hata kugundua kuwa ili uuze kazi yako inaanzia kwenye muonekano kwa kulitambua hilo alimgundua bingwa wa makava Bongo Raqey na kumpatia kazi hiyo.
Hadi sasa ili msanii mkubwa filamu yake iweze kuingia sokoni kwa uhakika lazima kava lake litengenezwa I View Media, lakini Ray amekuwa akigundua vipaji vipya kila leo na kuvipa uhusika jambo ambalo limezidi kuongeza wasanii katika tasnia ya filamu, mambo ni mengi kutoka kwa mtu huyu.
 |
the second wife |
Lakini ndiye msanii pekee ambaye hata ukimkosoa anaweza kutumia busara kuongea na wewe na kujadili jambo husika, kulingana na mfumo uliopo unawabana sana wasanii kujitanua zaidi kimaslahi jambo ambalo linapunguza utendaji wao, bila uoga wala chuki tunasema kuwa Bila Ray Hakuna Bongo movie kwa maana ya filamu.