SULTAN TAMBA NA KILIO CHA BODI YA UKAGUZI WA FILAMU.

Katika kupita pita kwenye kurasa za kijamii leo asubuhi bongo film data base ikakutana na mambo mengi sana juu ya tasnia hii ya filamu hapa Tanzania,  ila mwandishi na mwongozaji wa filamu hapa nchini bwana Sultan Tamba alikuwa na haya machache ila mazito kutoka kwenye nafsi yake juu vikwazo alivyopitia kuaanda kazi zake alipojaribu kufuata taratibu za kisheria na lingine kubwa zaidi ni juu ya BODI YA UKAGUZI WA FILAMU  kuziamsha sheria zake ambazo zinaonekana kukera wengi kwa namna moja ama nyingine...
Tamba alizungumza haya kupitia ukumbi wa maoni ndani ya ukurasa wake wa  facebook..
  Sultan; ''BODI YA UKAGUZI WA FILAMU imeanza mipango kabambe ya kuua filamu za kibongo. Kupitia sheria yao mpya, wametunga kanuni kwamba kutengeneza filamu kuanzia sasa ni lazima kwanza upeleke bodi mswada (script) yako na SH. LAKI TANO - unapewa kibali cha miezi mitatu, ukiwa na haraka wamesema ulipe MILIONI MOJA! Ukimaliza kutengeneza peleka wakaikague na ULIPE 60,000! Na mnajua ukaguzi wao ulivyo? Filamu yangu ya KESI YA JINAI ilikaa ofisini kwao MWAKA MZIMA wananizungusha tu! Zingine wanazikataa kwa sababu za ajabu ajabu sana. Hii kitu ni ya kuijia juu, wanaua tasnia, lakini tatizo UMOJA HATUNA! Kila mtu anafikiria tumbo lake binafsi. Ila habari ndo hiyo, sheria imeshaanza kazi na kuna kufungwa kama ukikaidi!
 
 SWALI ; Je?!  WATUMISHI WA BODI YA UKAGUZI WA FILAMU HAPA NCHINI WANA KISOMO CHA KUTOSHA JUU YA MAJUKUMU YAO????
BONGO FILM DATA BASE ITAKULETE MAONO YA WADAU MBALI MBALI WA FILAMU JUU YA SHERIA MPYA ZA  UTAYALISHAJI FILAMU HAPA NCHINI .
Asante!

Posted by Bongo Film Data Base on 11:24 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for SULTAN TAMBA NA KILIO CHA BODI YA UKAGUZI WA FILAMU.

Post a Comment

LETS HOOK UP

.

.
.
slide

SIRI YA MTUNGI PHOTO CAPTION

Recently Commented

ALBUM YA BONGOFILM

SIMULIZI ZILIZOBAMBA KWENYE KURASA ZA KIJAMII

TAKE ONE -HBABA NA FLORA INTERVIEW

2009 Bongofilmdatabase. All Rights Reserved. - Designed by Oscar kwa ushirikiano wa SimplexDesign