WASANI WAUNGANA NA KUTOA TAMKO RASMI JUU YA SHERIA MPYA ZA UTAYARISHAJI FILAMU NCHINI

Chama cha waaigizaji nchini kupitia waakirishi wake waishio mkoani dar es salaam waliokutana jana tarehe kumi na sita kwenye mkutano ambao uliyotakiwa ufanyike tarehe kumi na mbili na kuhailishwa kutokana na msiba ulioikumba tasnia ya filamu kumpoteza mzee na mwasisi bwana saidi fundi ( mzee kipara).

Awali wa yote bongo Film Data Base  tunaipongeza  bodi ya ukaguzi filamu  hapa nchini kwa namna moja ama nyingine  kuwaleta wasanii  taklibani wote kwa pamoja na wao kusahau tofauti zao za nyuma zilizo kuwa zikifukuta kwa chini chini kati yao yaani wasanii waliokuwepo Tanzania Film Federation (Taff) na wasanii waliopo Bongo Movie ,mh! kumbe mambo yakimfika mtu hulazika kutafuta nguzo ya kusimami na yeye apate ulinzi wakutosha nakupaza sauti yake enh?!

Haya wadau wa tasnia hii ya maigizo twendeni kazi sasa na tuache mambo haya ya bifu na mpasuko kwani hayana nguvu kupinga hoja za msingi kama hizi za kisheria kutoka serikalini sisi twasema  na kusisitizia juu ya hili tu ajamani ila huu ni wakati sasa wakutumia nguvu zenu nyingi na busara yakotosha  kufanikisha  hili na kujiwekea mazingira mazuri ya ufanyaji kazi zenu...twendeni moja kwa moja kwenye lile lililojiri hapo ukumbi wa vijana.

  Kikao kilianza saa tatu asubuhi na  kwa mujibu wa taarifa za awali zilizosambazwa na chama cha waigizaji mkoa wa dare es salaam  kwa uma kupitia vyombo vya habari mbali mbali ukiwemo ukurasa huu wa Bong film Data Base.awali wa  kikao hicho kilitawaliwa na kejeri,dharau na majigambo kutoka  kwa  baadhi ya wasanii walipo simama kuchangia mada zilizotolewa, hali ilikuwa si shwari kabisa kwa kila aliye simama kuzungumza lolote kuhusiana na jambo hili, aliyechangia  alitoa kauli moja tu '' KANUNI NA SHERIA HIZI HAZIFAI NA  HATUZITAKI!!''

Kauli hii imtoka kila aliye sisima kuzungumzia hili tena ikiwa katika hali ya jaziba nzito sana, baada ya muda fulani mambo yalitulia kwenye majira ya mchana baada ya kila mmoja kuzipitia kanuni na sheria hizi vizuri ambazo zilizokuwa zimechapishwa kwenye karatasi kadhaa na kugawiwa kwa idadi kubwa ya wasanii waliokuwa wamefika nyakati za asubuhi pale kikao kilipokuwa kinaanza.

Mara baada ya hali kuwa shwari sasa na wasanii kuanza kuzungumza bila jaziba  walizungumza mengi sana kuhusiana na Bodi ya Filamu,Basata na Cosota kama ifuatavyo;

WAENDESHA KIKAO HIKI TOKA MEZA KUU AMBAPO MWENYEKITI WA KIKAO HIKI BWANA MIKE SANGU ALIREJEA NA KUZIELEZEA KWA UFUPI KANUNI NA SHERI HIZI MARA KWA MARA, KIPENGELE CHA GHARAMA KILIONEKANA NDICHO KILIWARUSHA ROHO NA KUWAOGOPESHA WENGI ZAIDI...

MIKE SANGU  ALILAZIMIKA KUFAFANUA KIPENGELE CHA GHARAMA TENA KAMA IFUATAVYO;

 Bodi ya ukanguzi filamu nchini kukagua flamu Gharama ya ukaguzi kwa saa moja ni shilingi elfu sitini (60,000) za kitanzania kwa kawaida na shilingi laki moja (100,000) kwa haraka zaidi  za hizi ni gharama hutumika kwa watayarishaji filamu wa ndani ya nchi na watayarisha wa kigeni hulipa dola za kimarekani hamsini 50$

 kibari cha upigaji picha hutolewa kwa wazawa kwa shilingi laki tano (500,000) na kwa wageni itawagharimu dola elfu moja (1000$)

 Gharama zipo nyingi zilizoainishwa kwenye kanuni na sheria hizi ikiwemo na shilingi elfu tano (5'000) kwa kila chapisho la tangazo litakalo bandikwa mtaani litangazalo filamu ama kazi ya aina yeyeto ya sanaa (poster)

Mh! wacha nigune kimya kimya mie, maana kelele zilivyoibuka kila pembe ya ukumbi wa vijana pale kinondoni ilikuwa si mchezo.....

WASANII NAO WALIKUWA NA HAYA 

John Rister;
  •      Bodi ya ukaguzi filamu  ni chombo kikubwa sana kuongozwa na watu sita tu ni makosa makubwa sana, hivyo serikali anafungua milango mingine mipya ya wala rushwa kwani hawa watumishi wake sita tu hawawezi kukagua miswada(script) na filamu zilizo kwisha tayarishwa na watayarishaji zadi ya mamia ndani ya mwezi mmoja.
  • Bodi ya Filamu inaingilia kazi za mamlaka ya ukusanyaji kodi nchini (TRA)
  •                (SHERIA NA KANUNI HIZI  HAZITUFAI!)   
  •                 
Single Mtambalike;
  • Bodi ya ukaguzi wa filamu kukagua kazi zetu ni jambo zuri, la msingi na itaonesha ukomavu wa tasnia yetu ila nina shaka kubwa sana kama jopo hili la hapo bodi ya ukaguzi wa filamu na idadi yao hiyo ya watu sita kama wataweza kuacha ofisi yao na kuungana nami kwenda kukagua eneo ninalo kwenda kupigia picha huko mwanza ama tanga vijijini...si dhani!! waache kutudanganya..
  • Bodi inafanya kazi zinazotakiwa kufanywa na shirikisho la filamu nchini (Taff) 
  •               (SHERIA NA KANUNI HIZI  HAZITUFAI!)



Myovela Mfwaisa;

  •    Serikali tulionayo leo hii ndiyo ile iliyokuwepo miaka kumi hadi kumi na tano ilyopita hali kadharika sheria na kanuni hizi zilikuwepo pia, swali la kujiuliza hapa kwanza ni kwamba!,kwanini hawakuzipa mpawa na nguvu kiasi hiki siku za nyuma?
  • mie na weza sema  wasambazaji filamu nchini ndiyo chanzo wa yote haya tunayoyaona kwa sasa, wasambazaji huingiza filamu nne hadi tano ndani ya mwezi mmoja na zote kufanya vizuri sokoni hivyo nilazima serikali itizama vizuri kona hii..kiukweli mie sishangai kuona hili, serikali inataka kodi na mapato yake yaongezeke jamani!
  •    (SHERIA NA KANUNI HIZI  HAZITUFAI!)


Chikoka;
  •     mimi binafsi nazikataa gharama  zote zilizopo kwenye sheria na kanuni hizi kutoka Bodi ya filamu.
  • kanuni hizi kiukweli zinatugandamiza na kamwe hatuta kwenda popote pale zaidi ya kuchezea sakafu ya hapa Tanzania, mfano mie nina rafiki yangu kutoka nchini India atashindwa kuja kufanya kazi hapa nchini na mwishoe kazi zetu hazita kwenda mataifa ya wenzetu kamwe!
  •  
                                          (SHERIA NA KANUNI HIZI  HAZITUFAHI!)
Chiki;
  • sheria na kanuni hizi ni batili kwenu kwani hatujashirikishwa kwenye utayarishaji wake.
                                     (SHERIA NA KANUNI HIZI  HAZITUFAI!)

Kanumba;
  • Bodi ya Filamu yapaswa kuundwa na baadhi ya viongozi wa Taff na bila ya kuwa hivyo mimi sina imani na bodi ya filamu kabisa...
  • mimi nina kampuni yangu ambayo nimesajari kunako husihuka na ninalipa kodi TRA hivyo sielewi  bodi natakiwa kuwalipa nini?
  • kwa upande wa kumomonyoka kwa maadili ya mtanzania kupitia filamu mimi na pingana nao kabisa kwani msanii anapovaa nguo fupi kwenye filamu ni kwa sababu amepaswa kuvaa hivyo kulingana na uhusika anaocheza na kulingana na mswada(script) unamtaka acheze.
  • kama kweli bodi ya filamu ina nia nzuri na tasnia hii ya filamu hapa nchini ni vyema kabisa ila walipaswa kuanza na kurudisha majumba ya sinema yalikuwepo sik za nyuma ambayo yalikufa kutokana na sheria na kanuni kali..
  •          (SHERIA NA KANUNI HIZI  HAZITUFAI!)  

Chaiba Kombo;
  •    Bodi ya Filamu inaingilia kazi zisizo wahusu kabisa
  • Na je? sheria hizi zimetizamwa kimataifa?
  • Yote haya yanawaumiza vichwa wasanii kwa sababu yakutokuwa na elimu nzuri juu saana wanaoifanya.
  • wasanii hawakushirikishwa kwenye uundaji sheri na kanuni hizi...
  • (SHERIA NA KANUNI HIZI  HAZITUFAI!)

HITIMISHO LA MKUTANO HUU TOKA MEZA KUU;
 1.Tutaiandika barua Bodi ya ukaguzi filamu nchini kupinga sheri na kanuni hizi kwa hoja zote zilizokusanywa kwenye mkutano huu.
2. hatuitambui bodi hii kwani haijahusisha watu wahusika kwa maana ya wasanii toka kwenye shirikisho letu hivyo bodi ivunjwe na kuundwa upya tena.

(SHERIA NA KANUNI HIZI  HAZITUFAI!) (SHERIA NA KANUNI HIZI  HAZITUFAI!)!!!!!

Posted by Bongo Film Data Base on 12:25 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for WASANI WAUNGANA NA KUTOA TAMKO RASMI JUU YA SHERIA MPYA ZA UTAYARISHAJI FILAMU NCHINI

Post a Comment

LETS HOOK UP

.

.
.
slide

SIRI YA MTUNGI PHOTO CAPTION


Recently Commented

ALBUM YA BONGOFILM

SIMULIZI ZILIZOBAMBA KWENYE KURASA ZA KIJAMII

TAKE ONE -HBABA NA FLORA INTERVIEW

2009 Bongofilmdatabase. All Rights Reserved. - Designed by Oscar kwa ushirikiano wa SimplexDesign