UWOYA; MAISHA MAGUMU SANA

BAADA ya misukosuko ya ndoa yake, Irene Pancras Uwoya (pichani), amekiri kuwa sasa maisha ni magumu kuliko alivyokuwa akiyafikiria.
Akizungumza na mwandishi wetu jijini Dar es Salaam juzikati, Irene aliweka wazi kuwa hajawahi kupitia maisha ya ukata kama anayokumbana nayo hivyo ameanza kuwa makini katika matumizi ya kile anachopata.

“Asikwambie mtu, nimeonja joto ya jiwe, nimeamua kupunguza matumizi yote yasiyo ya lazima ili angalau niende sawa na maisha haya,” alisema Uwoya ambaye ni kichwa cha mauzo katika muvi za Kibongo.

Staa huyo aliyetamba vilivyo katika Filamu ya Dj Ben inayosumbua sokoni, amewataka mastaa wenzake kuwa na nidhamu ya fedha kwani zikiondoka zinatoweka moja kwa moja.

Posted by Bongo Film Data Base on 9:59 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for UWOYA; MAISHA MAGUMU SANA

Post a Comment

LETS HOOK UP

.

.
.
slide

SIRI YA MTUNGI PHOTO CAPTION


Recently Commented

ALBUM YA BONGOFILM

SIMULIZI ZILIZOBAMBA KWENYE KURASA ZA KIJAMII

TAKE ONE -HBABA NA FLORA INTERVIEW

2009 Bongofilmdatabase. All Rights Reserved. - Designed by Oscar kwa ushirikiano wa SimplexDesign