HISSAN MUYA KIJANA NA MWIGIZAJI MWENYE NAFSI YA KUTHUBUTU AJA NA GONGOLAMBOTO SASA BAADA YA KUSHIDWA KUFANIKISHA NA FILAMU ZAKE ZA SHOGA NA LOLIONDO


FILAMU ya kipekee na aina yake ya Gongolamboto ipo tayari na inaingia sokoni mwezi huu wa tatu filamu hiyo inasambazwa na kampuni ya Steps Entertainment Ltd wasambazaji wakubwa wa kazi za filamu Swahiliwood, filamu ya Gongolamboto ‘Usiku wa Heka heka’ ni filamu iliyoandikwa na mwandishi mahiri wa muswada Tanzania Octavian Vitalis ‘Octa’ na kuigizwa na magwiji wa tasnia hii ya filamu Tanzania.


Akiongea na FC mtayarishaji na mwandishi wa filamu hiyo Octa amesema kuwa filamu hiyo imerekodiwa katika mkoa wa Morogoro huku lengo kubwa likiwa ni kutoa fursa kwa wasanii wachanga kutoka katika mkoa huo na kupanua tasnia hiyo kwa kusonga mbele zaidi walioshiriki katika filamu hiyo ni Muhogo Mchungu, Tino, Otilia Joseph, Muhogo Mchungu aliongelea filamu hiyo kwa ufupi.
“Filamu hii ya Gongolamboto ni kazi ambayo imenileta upya katika tasnia ya filamu ni kazi ambayo hata wakati naigiza nilikuwa nasikia raha na kuhisi mwandishi wa filamu hii kama alikuwa ndani ya akili yangu na kunipa uhusika ulioendana na mimi kabisa napenda kutumia nafasi hii kumpongeza sana Octa na waandishi wengine waige mfano wake wakuandika hadithi zetu,”anasema Muhongo Mchungu.

Chanzo;filamu centralPosted by Bongo Film Data Base on 1:51 PM. Filed under , , , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for HISSAN MUYA KIJANA NA MWIGIZAJI MWENYE NAFSI YA KUTHUBUTU AJA NA GONGOLAMBOTO SASA BAADA YA KUSHIDWA KUFANIKISHA NA FILAMU ZAKE ZA SHOGA NA LOLIONDO

Post a Comment

LETS HOOK UP

.

.
.
slide

SIRI YA MTUNGI PHOTO CAPTION

Recently Commented

ALBUM YA BONGOFILM

SIMULIZI ZILIZOBAMBA KWENYE KURASA ZA KIJAMII

TAKE ONE -HBABA NA FLORA INTERVIEW

2009 Bongofilmdatabase. All Rights Reserved. - Designed by Oscar kwa ushirikiano wa SimplexDesign