SWAHILI FILM AWARDS 2012 ZAJA KWA MARA NYINGINE TENA ,SASA KUUTAMBUA UBORA NA UMOJA WA KAZI ZA WASANII

Ni miaka 50 sasa tangu Mtanzania asheherekee kupata Uhuru wa chi yake. Hii ni miaka ya kujivunia, iliyojaa historia kubwa ya maendeleo, mapambano na changamoto za kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiteknohama katika maisha ya Mtanzania. Utamaduni ni Uti wa mgongo wa Mtanzania…. Hii ni kauli maarufu ya Rais wa kwanza wa Tanganyika Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyoitoa siku chache tu baada ya kupata Uhuru.

Swahilifilm awards 2012
Filamu ni moja ya njia za kuzitunza, kuzilinda na kuziendeleza tamaduni zetu. Na huu ni muda muafaka kwa kuwatunuku watayarishaji, waigizaji, waongozaji wa filamu, wahariri na wadau wote wa tasnia ya filamu Swahiliwood.

SWAHILI FILM AWARDS inatambua UBORA na UMOJA uliopo na unaohitajika ili kukuza tasnia hii ya filamu Tanzania, ni wakati wako wa kuwakilisha kazi yako ambayo ilitoka mwaka uliopita yaani mwaka 2011 kwa ajili ya kuingia katika tuzo kubwa na za kwanza kufanyika Swahiliwood kwa maelezo zaidi unaweza kutembelea mtandao wa www.swahiliawards.co.tz

Ni msimu wa furaha na kufuta machungu baada ya kutambuliwa kazi unayofanya huku tukizingatia kujenga UBORA na UMOJA wa kweli katika kujenga na kukuza tasnia hii ya filamu inayokua kwa kasi kubwa na kuleta tija tupo pamoja fomu zinapatikana kupitia mtandao lakini pia unaweza kuzipata sehemu kama Redio Uhuru Fm, kwa Wasambazaji wote na kwa maafisa Utamaduni nchini kote.
Posted by Bongo Film Data Base on 1:11 PM. Filed under , , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for SWAHILI FILM AWARDS 2012 ZAJA KWA MARA NYINGINE TENA ,SASA KUUTAMBUA UBORA NA UMOJA WA KAZI ZA WASANII

Post a Comment

LETS HOOK UP

.

.
.
slide

SIRI YA MTUNGI PHOTO CAPTION

Recently Commented

ALBUM YA BONGOFILM

SIMULIZI ZILIZOBAMBA KWENYE KURASA ZA KIJAMII

TAKE ONE -HBABA NA FLORA INTERVIEW

2009 Bongofilmdatabase. All Rights Reserved. - Designed by Oscar kwa ushirikiano wa SimplexDesign