JE! BODI YA UKAGUZI WA FILAMU HAPA NCHINI NI SEHUMU YA SERIKALI AU NI WAJASIRIAMALI?

''Eti Bodi ya Ukaguzi wa Filamu nchini inatoza shilingi 500,000/= za ukaguzi wa filamu husika. Naona wamebadili kutoka kuwa bodi ya ukaguzi wa filamu hadi ujasiriamali, makubwa hayo Lol...''
 Na Markus Mpangala kupitia ukuta wake wa mtadao wa kijamii facebook.



Posted by Bongo Film Data Base on 4:37 PM. Filed under , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

1 comments for JE! BODI YA UKAGUZI WA FILAMU HAPA NCHINI NI SEHUMU YA SERIKALI AU NI WAJASIRIAMALI?

  1. Kimsingi ukaguzi wa filamu yoyote unasimamiwa na sheria. Siyo lazima sheria ichukue mkondo wake kwa kuidhinishwa na fedha. Nafikiri ili kutoa huduma ya kukagua filamu nchini lazima tufahamu kuwa kuna tofauti kati ya kukagua na kulipia huduma ya ukaguzi. Ukaguzi unafanywa kwa mujibu wa sheria. lakini kulipia huduma ya ukaguzi wa filamu maana yake bodi ya filamu inapanga ada ya ukaguzi ili filamu iruhusiwe. kwahiyo ada ya 500,000/= kwa filamu zetu, mtaji wa kutengeneza filamu, vifaa na kadhalika siamini kuwa wasanii au watenegeneza filamu wanao uwezo mkubwa kama wengine wa nje. Tatizo ni kwamba, bodi ya filamu inadhani nguvu ya ada kubwa ya ukaguzi wa filamu ni kigezo cha kupelekewa filamu bora. Bodi inasahau kuwa ipo kwa mujibu wa sheria. na makosa ya kwenye filamu yanatolewa adhabu kwa mujibu wa sheria siyo kiwango cha ada. Ninavyoona hapa Bodi ya Filamu inadhani kiwango cha ada ni kigezo cha kutotengenezwa filamu mbovu.

    BODI YA FILAMU IFANYE NINI?
    Kwanza lazima ikubali ndio yenye mamlaka ya ukaguzi kwa mujibu wa sheria. Pili ifahamu mzingira ya utengenezaji wa filamu nchini kwamba idadi kubwa ya wasanii au watengenezaji sio wenye mitaji mikubwa. kwahiyo kiwango cha ada hakina nguvu kuliko sheria.
    sheria inasimamia suala zima la filamu, kwahiyo ada ya ukaguzi inakuwa haina nguvu yoyote ingawa ni muhimu.
    kwahiyo bodi inapaswa kuweka uwiano wa ukaguzi wa filamu kulingana na majukumu(maeneo ya ukaguzi) pamoja na sheria zinazoongoza. pia tatizo sio laki tano tu bali maelezo juu ya ukaguzi. huwezi kuwatoza watu ada ya kuangalia(kuketi na kukagua) kwa shilingi wakati sheria na ada ya ukaguzi ipo. mchanganuo wa ukaguzi hauleti manufaa yoyote zaidi ya ujasiriamali unavyofanywa. bila kubadili viwango na sababu za viwango vya ukaguzi, basi hakuna tofauti kati ya Bodi ya Filamu na wachuuzi

Post a Comment

LETS HOOK UP

.

.
.
slide

SIRI YA MTUNGI PHOTO CAPTION


Recently Commented

ALBUM YA BONGOFILM

SIMULIZI ZILIZOBAMBA KWENYE KURASA ZA KIJAMII

TAKE ONE -HBABA NA FLORA INTERVIEW

2009 Bongofilmdatabase. All Rights Reserved. - Designed by Oscar kwa ushirikiano wa SimplexDesign