Emmanuel John; UTENGENEZAJI FILAMU ZENYE VINGO HAPA BONGO TUANAHITAJI FEDHA AU NI ELIMU?

Mimi huwa nashangazwa na kitu kimoja, kila Msanii anayepata nafasi kwenye media, akiulizwa nini kifanyike kusadia tasnia ya filamu wote utawasikia, Serikali idhibiti Piracy, Raisi aingilie kati uharamia, Je ni kweli tatizo la Filamu zetu ni mauzo peke yake ? Je wasanii hawa wanaridhika na filamu wanazozitengeneza mpaka kufikia kutamani kuuza kopi milioni moja? au ni kwa kuwa washabiki wetu wananunua chochote tunachowatengenezea ? Mimi nadhani kitu ambacho wanatakiwa kuomba kwa Mheshimiwa raisi ni, Atutafutie mwalimu wa ACTING FOR THE CAMERA aje hapa nchini kupunguza gharama.
 PILI tunahitaji kuwa na DIRECTORS OF PHOTOGRAPH kwa ajili ya kutengeneza filamu na sio CAMERA MAN tu. watu kama ADAM JUMA watengenezwe wa kutosha, Wasanii wote wanatamani kuuza kopi milioni moja, fine sina ugomvi na hilo. lakini hata kwa kile kidogo wanachopata wanakifanyia nini zaidi ya kununua magari ya kifahari na matanuzi ya kufuru ? Wanashindwa nini kutenga pesa hizo kidogo kuendea shule ya ACTING ? 
Msanii kama Ray na wengine wengi hukosi milioni ishirini kwenda kusoma ? Hata mkipata hayo mabilioni mnayotamani tutarajie nini zaidi ya magari na starehe ? Hivi hata siku moja wasanii hatutamani kufanya kama kina MARTIN LAWRENCE, TICHINA ANORLD kutaja wachache, je tunadhani kuifikia levo ya wasanii hawa inatokea tu kama miujiza au kutengeneza msururu wa filamu ? Tufikie mahali tunatengeneza filamu moja kwa mwaka lakini ni ya Ukweli. HAKUNA LISILOWEZEKANA, Martin sio malaika na tunaweza kuwa na akina Martin Lawrence na Tichina Arnold wetu nchini (ila wanaandaliwa)
 Na.  Emmanuel John kupitia ukurasa wake wa Facebook.
 
 
 
kama utakuwa na mawazo au jambo la kusema kuhusiana na tasnia hii tafadhali tutumie taarifa au habari nasi tutazi chapa.
Asante!

Posted by Osxarguder • The Creator • on 5:19 PM. Filed under , , , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

1 comments for Emmanuel John; UTENGENEZAJI FILAMU ZENYE VINGO HAPA BONGO TUANAHITAJI FEDHA AU NI ELIMU?

Post a Comment

LETS HOOK UP

.

.
.
slide

SIRI YA MTUNGI PHOTO CAPTION

Recently Commented

ALBUM YA BONGOFILM

SIMULIZI ZILIZOBAMBA KWENYE KURASA ZA KIJAMII

TAKE ONE -HBABA NA FLORA INTERVIEW

2009 Bongofilmdatabase. All Rights Reserved. - Designed by Oscar kwa ushirikiano wa SimplexDesign