Emmanuel John; UTENGENEZAJI FILAMU ZENYE VINGO HAPA BONGO TUANAHITAJI FEDHA AU NI ELIMU?
Posted by bongofilmdatabase
habari,
habari...,
mtandao,
slide
5:19 PM
Mimi
huwa nashangazwa na kitu kimoja, kila Msanii anayepata nafasi kwenye
media, akiulizwa nini kifanyike kusadia tasnia ya filamu wote
utawasikia, Serikali idhibiti Piracy, Raisi aingilie kati uharamia, Je
ni kweli tatizo la Filamu zetu ni mauzo peke yake ? Je wasanii hawa
wanaridhika na filamu wanazozitengeneza mpaka kufikia kutamani kuuza
kopi milioni moja? au ni kwa kuwa washabiki wetu wananunua
chochote tunachowatengenezea ? Mimi nadhani kitu ambacho wanatakiwa
kuomba kwa Mheshimiwa raisi ni, Atutafutie mwalimu wa ACTING FOR THE
CAMERA aje hapa nchini kupunguza gharama.
PILI tunahitaji kuwa na
DIRECTORS OF PHOTOGRAPH kwa ajili ya kutengeneza filamu na sio CAMERA
MAN tu. watu kama ADAM JUMA watengenezwe wa kutosha, Wasanii wote
wanatamani kuuza kopi milioni moja, fine sina ugomvi na hilo. lakini
hata kwa kile kidogo wanachopata wanakifanyia nini zaidi ya kununua
magari ya kifahari na matanuzi ya kufuru ? Wanashindwa nini kutenga pesa
hizo kidogo kuendea shule ya ACTING ?
Msanii kama Ray na wengine wengi
hukosi milioni ishirini kwenda kusoma ? Hata mkipata hayo mabilioni
mnayotamani tutarajie nini zaidi ya magari na starehe ? Hivi hata siku
moja wasanii hatutamani kufanya kama kina MARTIN LAWRENCE, TICHINA
ANORLD kutaja wachache, je tunadhani kuifikia levo ya wasanii hawa
inatokea tu kama miujiza au kutengeneza msururu wa filamu ? Tufikie
mahali tunatengeneza filamu moja kwa mwaka lakini ni ya Ukweli. HAKUNA
LISILOWEZEKANA, Martin sio malaika na tunaweza kuwa na akina Martin
Lawrence na Tichina Arnold wetu nchini (ila wanaandaliwa)
Na. Emmanuel John kupitia ukurasa wake wa Facebook.
kama utakuwa na mawazo au jambo la kusema kuhusiana na tasnia hii tafadhali tutumie taarifa au habari nasi tutazi chapa.
Asante!
you are in point of fact a just right webmaster.
The website loading velocity is amazing. It
sort of feels that you're doing any unique trick. Also, The contents are masterpiece. you've done a fantastic job in this subject!
Also visit my web blog Oregon mortgage help