WAONGOZAJI FILAMU WATANO BORA KWA SASA NI HAWA HAPA


1. James Francis Cameron

alizaliwa tarehe 16 mwezi wa nane munamo mwaka 1954 hapo Kapuskasing Ontario, nchini Canada.baada ya miaka kadhaa kidogo alihamia united State kwenye miaka ya 1971.baab yake alikuwa mkandarasi na mazingira hayo yalimpelekea James naye anfuata nyayo za baba yake na kuhitimu masomo ya phizikia chuo kikuu cha hapo mji wa California. Pamoja na kuhitimu elimu yake hiyo ya juu ya mambo ya kisayansi james aliamua kwenda kuishi kwenye ndoto zake za siku nyingi za uandishi miongozo ya sinema kwa jina la kitaalamu muswada(script)

hizi hapa ni baadhi ya filamu zake zilizomtambulisha vyema
 

2. Steven Soderbergh 
Peter Soderbergh profesa na mkuu wa chuo cha elimu hapo jimbo la  louisiana baba yake Steven  amaye ni mtoto wa pili kwenye uzazi wa watoto sita aliyezaliwa wa pale mji wa Atlanta,Georgia Marekani munamo mwaka 1963 tarehe 14 mwezi wa kwanza,Steven akiwa bado mdogo familia yake wote walihamia Baton rouge Louisiana kule baba yake alikuwa mkuu wa chuo. kipindi bado yupo shule ya upili akiwa ana umri wa  miaka 15 akajiunga kwenye chuo cha mambo ya sinema na kuhudhulia vipindi vya utengenezaji katuni na kuanza kutengeneza filamu fupi kwa kutumia vifaa chakavu, moja ya filamu zake hizo ni ''Janitor'' mara baada ya kuhitimu masomo yake ya ngazi ya upili alikwenda hollywood na kufanya kazi za uhariri za bila kuajiriwa ingawa alikaa muda mfupi sana huko hollywood aliutumia ipasavyo muda huyo mdogo kwa nafasi hiyo aliyoipata, alirejea nyumbani na kuendelea na kutengeneza filamu fupi.  

hizi hapa ni baadhi ya filamu zake zilizomtambulisha vyema
 
 3. Robert Rodriguez 
 
alizaliwa na kulelewa kwenye mji wa San Antonio huko Texas Marekani, akiwa bado mdogo aliionesha familia yake yeye kuvutiwa na kupenda sana kutengeza katuni na filamu hivyo akautenga muda wake kukiendeleza kile kilimgusa rohoni na hatimaye shughuli hiyo ikamlipa  kulikompelekea anze kutengeza filamu kubwa kubwa na moja ya filamu hizo za awali ilikuwa ni Eli-marachi ya mwaka 1992

 
Eli-marachi
na filamu hii ilimwekea mazingira mazuri na kumwongezea jina kama mtayarisha bora aliyetayarisha filamu kwa kutumia fedha kidogo sana. kitu ambacho kilmkuza Robert ni hile hali ya kijiamini na kiuwa na roho ya kuthubutu pale alidhani anaweza kufanya jambo. baada ya hapo aliweza kuandika kuongoza,kuhariri,na hata kutayarisha vyema zaidi tofauti na pale awali filamu kama kumi na mbili hivi zikiwemo Desperado ya mwaka 1995, From Dusk Till Dawn ya mwaka 1996, The Faculty ya mwaka 1998 na Spy kids ya mwaka 2001 

hizi hapa ni baadhi ya filamu zake zilizomtambulisha vyema
 


4. Matt Reeves 
mwandishi ,mwongozaji na mtayarishaji wa filamu huko hollywood aliye shirikiana na J.J. Abrams kwa mara ya kwanza kwenye utayarishaji filamu fupi pale Los Angeles, Matt Reeves alizaliwa mwezi wa nne munamo mwaka 1966 mjini Rockville Centre, New York nchini Marekani.

hizi hapa ni baadhi ya filamu zake zilizomtambulisha vyema
 

5. Neill Blomkamp 
mzaliwa wa hapo bondeni kwa Madiba mjini Johannesburg nchini Afrika kusini alihitimu mafunzo ya utengenezaji katuni kwenye mfumo wa 3D na utengenezaji sauti mwanga na rangi za filamu kitalaamu mwaka 1998 na kuhamia nchini Canada akiwa ana umri wa miaka 18 tu na kupata nafasi ya kazi upande wa uteuzi wasanii kwenye kampuni moja iliyojihusisha na uchapaji jarida  lililo kwenda patiakana mtaani kwa jina la Time magazine's jarida hili likuwa mahususi kwa kuzungumzia watu mahiri duniani kabla hajaanza kujihusisha rasmi na utayarishaji filamu. 

hizi hapa ni baadhi ya filamu zake zilizomtambulisha vyema

 
 
Na. Mwandishi Wetu 
kwa kushirikiana 
na 
Emmanuel M.M. Manase kupitia ukurasa wa TFCA

Posted by Osxarguder • The Creator • on 1:57 PM. Filed under , , , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for WAONGOZAJI FILAMU WATANO BORA KWA SASA NI HAWA HAPA

Post a Comment

LETS HOOK UP

.

.
.
slide

SIRI YA MTUNGI PHOTO CAPTION

Recently Commented

ALBUM YA BONGOFILM

SIMULIZI ZILIZOBAMBA KWENYE KURASA ZA KIJAMII

TAKE ONE -HBABA NA FLORA INTERVIEW

2009 Bongofilmdatabase. All Rights Reserved. - Designed by Oscar kwa ushirikiano wa SimplexDesign