MJUE VILIVYO HASHIM KAMBI


Kama unafuatilia sanaa ya filamu nchini Tanzania, sina wasiwasi kwamba sura unayoiona hapo juu unaitambua. Unachoweza kuwa hukijui ni jina lake kwa sababu pamoja na kwamba yeye ni miongoni mwa wasanii katika tasnia ya filamu ambao tunaweza kuwaweka katika lile kundi la “wasanii makini”,bado yeye hupenda kubakia low profile.

Bila shaka utakubaliana nami nikisema uigizaji wake ni  ule ambao hauna papara.Pengine hii inatokana na nafasi(roles) anazopatiwa na kuzikubali lakini binafsi naamini ni kipaji cha uigizaji alichonacho.
Jina lake ni Hashim Kambi.

Kambi alizaliwa tarehe 21/10/1961(muda mfupi kabla ya Uhuru) huko mkoani Morogoro na alianza uigizaji mwaka 1999 baada kuchaguliwa na msanii Single Mtambalike ” Ritchie” kushiriki katika igizo lililoitwa Uhondo wa Ngoma uliorushwa na kituo cha Televisheni cha TVT kwa sasa TBC1. Huo ndio ukawa mwanzo wake katika fani ya uigizaji. Mpaka hivi leo, Hashim Kambi ameshiriki katika filamu chungu mbovu zikiwemo;
SIMU YA KIFO, 
KIPUSA, 
THE LOST TWINS,
 KIPURI,
 ZUADISWA,
 HONEY MOON, 
SURPRISE, 
RIPPLE OF TEARS, 
MISS CALL, 
ROMANCE, 
20%FURAHA IKO WAPI,
 THE PASSION, 
DAMU YA MJOMBA,
 BWAGAMOYO,
 BINTI NUSA,
 SANDA NYEUSI,
 BABU SEYA,
 NGUVU YA MAPENZI, 
PENZI LA BABA,
 OLOPONG, 
SILENT KILLER, 
HUBA, 
MY FIANCEE BORN AGAIN,
PRETTY GIRL, 
DANGEROUS DEAL.
Kambi ambaye ameoa na kubarikiwa kupata watoto ana urefu wa 5:9ft.


chanzo bongo celeb.

Posted by Osxarguder • The Creator • on 9:59 PM. Filed under , , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for MJUE VILIVYO HASHIM KAMBI

Post a Comment

LETS HOOK UP

.

.
.
slide

SIRI YA MTUNGI PHOTO CAPTION

Recently Commented

ALBUM YA BONGOFILM

SIMULIZI ZILIZOBAMBA KWENYE KURASA ZA KIJAMII

TAKE ONE -HBABA NA FLORA INTERVIEW

2009 Bongofilmdatabase. All Rights Reserved. - Designed by Oscar kwa ushirikiano wa SimplexDesign