
Ruge Mutahaba Mkurugenzi mwendeshaji Clouds Media Group.
UTAWALA ni kipaji na hasa pale utakapogundua kuhusu uwezo wako, si
kila mtu anaweza kuwa mtawala na kuweza kufanikisha jambo linalokusudiwa
iwe katika jamii hata katika familia yako, lakini kuna watu wanaweza
kufanya hivyo leo nafikiri ni vema kumuongelea Mh. Ruge Mutahaba
mkurugenzi mwendeshaji wa Clouds Media Group.

Ruge akiwa na Mh. Vick Kamata na Mtayarishaji wa wimbo maalum wa Mboni Yangu
Hivi Ruge Mutahaba ni nani hadi watu wote wamsikilize?
Naamini kuwa ndio maswali mengi ambayo sisi wapenda majungu, tusiona
mazuri wala upendo akufanyiaye mtu mwingine wakati wa matatizo,
nimegundua kuwa chuki ujengwa na watu dhaifu na wabinafsi kutokana na
uvuvi wao pia kukosa ubunifu kwa yale wanayoyafanya katika jamii.

Wema Sepetu Mwigizaji Swahiliwood akiimba wimbo wa Mboni yangu.
Binadamu kama binadamu ana mapungufu yake, lakini usimhukumu kwa
sababu eti umemsikia mtu au jamaa yako akimshutumu kama ni mtu mbaya na
wewe kwa ujinga wako ukiendeleza chuki maneno ya hovyo kwa sababu tu ya
huyo aliyetengeneza uhasama huo, Ruge ndiye mtu pekee ambaye ana uwezo
wa kutoa msaada kwa kutumia kile alicho nacho, lakini sisi ubaki na
maneno yetu ya fitina na majungu tu na si kutoa hata kile kidogo tulicho
nacho.
Najua wengi mtasema kuhusu makala hii lakini ukweli unabaki pale pale
kuwa Bongo watu kama Ruge ni wachache sana lakini kwa sasa nahisi yupo
peke yake tu, nimeshuhudia harakati zake nyingi sana akichangia wananchi
mfano mafuriko yaliyotokea Morogoro kule Kilosa ni yeye tu ndio alibuni
na kuratibu zoezi ambalo pengine nilitegemea wazo lile kufanywa na
Serikali au taasisi yoyote ya kijamii.
.

Ali Kiba Msanii wa muziki kizazi kipya naye alikuwepo kutoa support kwa Sajuki.
Baada ya msiba wa nyota wa filamu kutokea maneno mengi yalisikika
kuhusu wizi wa michango ya fedha iliyotolewa lakini wengi walimtuhumu
Ruge kama mpigaji na kila sifa mbaya alitwishwa lakini kwa sababu
anatujua sisi Wabongo ambao maneno mengi bila vitendo alipotezea na
kukaa kimya lakini naamini kuwa hata katika nafsi yake alisema kuwa
kumsaidia mtu ni shida na lawama.
Lakini nakumbuka kuwa Mwalimu wangu aliwahi kunieleza kuwa hakuna
msaada utolewao bure lazima utalipia tu iwe kwa kujua au kwa kutojua
kuwa umelipa au bado, hili si jambo la kusahau, linapotokea jambo
linahitaji utatuzi kwetu kidogo hatuwezi kufanya hivyo, basi inapotokea
mtu kufanya ni vema kumuunga mkono kuliko shutuma hilo limetokea na
kuonyesha ni jinsi gani kila msanii anahitaji kufa na tai yake shingoni.
.

Dito, Amini, Afande Sele walikuwepo nao katika kumchangia Sajuki.
Waswahili usema kuwa Mungu hamfichi mnafiki ikifika ndugu yetu Sajuki
anaumwa na ilikuwa inatakiwa fedha kwenda kutibiwa nje ya nchi yaani
India, kila mwenye roho safi alitoa alichokuwa nacho pia waandishi
walijitahidi kuujulisha umma kama msanii huyo anaumwa na anahitaji
msaada wa matibabu, lakini michango ilikuwa ya kusuasua na hata yale
makundi yanasumbua Swahiliwood yaani Bongo Movie na TAFF yalichemka
kufanikisha.
.

Mtayarishaji Mtitu akiimba naye katika wimbo wa Mboni yangu.
Nilifanya juhudi kwa kila njia ili mradi tu Sajuki aweze kusaidiwa
uelewa ulikuwa mdogo sana, tuliishia kumpigia simu tu huku tukimpa
Sajuki matumaini hewa bila upatikaji wa hizo fedha, hata pale walipofika
viongozi wa kiserikali nao bado walikuwa nyuma kuhusu maamuzi au njia
ambayo ingetumika ili kupata fedha.
Kamati ziliundwa huku shutuma nazo zikitawala kila mtu akishidwa
kumwamini mwingine, hadi pale mgonjwa mwenye pamoja kuumwa alikata
shauri na kusema sisikii maneno majungu ya mtu nahitaji kumuona Ruge kwa
msaada wangu ili nipate kutibiwa, kweli alifanya juhudi hadi alionana
na Ruge Sajuki anasema kuwa alikaa na Ruge kwa muda mfupi alionyesha
uwezo wake kubuni na kuratibu tukio la kumwezesha kupata fedha.
“Nilimweleza Ruge nimekuja ndugu yangu unisaidie, nahitaji fedha kwa
ajili ya matibabu na siku zinavyozidi kwenda ndio naumia, hadi sasa
naona ahadi tu ndio nyingi lakini hazina uhakika wa kupata fedha,
nilikuwa nikiongea huku nikiwa na mke wangu na rafiki yangu
Dino,”anasema Sajuki.
Baada ya hapo ndipo Ruge alipomjibu kwa kusema kuwa anaguswa na
tatizo lake kwa sababu ameenda yeye atamsaidia kabla alifuatwa na
wasanii wengine lakini kutokana na wasanii kutokujitambua na kumuona
kama yeye ni mtu dhulumati ilimpasa kubaki kama mchangiaji mwingine tu
ambaye angeweza kutoa kiasi alicho nacho kwa upendo wake au kuguswa na
tukio hilo.
“Hivi sasa tunawaogopa sana nyinyi wasanii walikuja wenzako na
kuniomba lakini sikuwa tayari kufanya lolote lakini kwa sababu umekuja
mwenye sina budi kukusaidia na tukio hilo linaanza kuanzia sasa lazima
tujue tunapata hiyo fedha ya matibabu,”alisema Ruge.
.

Ester Bulaya, Dina Marios, Asma Makau wakiwa studio kwa ajili ya kuchangisha fedha za matibabu kwa ajili ya Sajuki.
Ruge alichofanya ni kubuni wazo haraka nalo lilikuwa kutumia wimbo
uliokuwepo katika filamu ya wasanii hawa yaani Sajuki na Wastara kutoka
katika filamu ya Mboni yangu kuimbwa na wasanii wapatao 27 wakijumlishwa
na Waheshimiwa Wabunge zoezi lilofanyika siku hiyo hiyo na kila mtu
alitii wito ikiwa ni Wabunge na wasanii wote hasa wa muziki kwanini Ruge
asiitwe Shujaa wa Maafa?
.

Mzee Yusuf akiimba wimbo wa Mboni yangu.
Pamoja na hayo jambo lakusitikisha ni ushiriki wa wasanii wenye
shughuli kwa maana ya waigizaji ni wasanii wane tu ndio waliotia sauti
katika wimbo wa Mboni yangu ambao ni Wema Sepetu, Zuwena Mohamed
‘Shilole’ na William Mtitu sambamba na mhusika Wastara hiyo inaonyesha
ni jinsi gani tulivyogawanyika lakini siku ya siku tutakuwa wakwanza
kusema Ruge kapiga hela tuache maneno haya ya kuwachafua watu wakati
sisi hatuwezi kitu.
Ukisoma tu habari au kusikiliza Redio hata Televisheni utagundua kuwa
wasanii wana matabaka makubwa ambayo hayawasaidii zaidi ya kuwatia
umaskini tena wa kujitakia, Dina alisema kuwa kuna na wasanii wa filamu
ambao wamekuwa wakijitoa hata uwaite saa nane za usiku watakuja ambao ni
Mtitu, Wema na Shilole hili ni tatizo.
.

Sajuki Mtayarishaji na Muongozaji wa filamu Swahiliwood.
Inawezekana kuna wasanii hawakuja kwa sababu hawakupigiwa simu
kutokana na uzito wao lakini pia wadau hata kama wasanii ni wazito
katika matukio ya kijamii tuwaite tu wasipokuja lakini ujumbe wamepata,
kwani nimeamua kumpongeza Ruge kwa kuwa mbunifu hata mimi ungenipa Redio
na Televisheni na kuniambia nifanye tukio litalomshawishi mtu
kuchangisha fedha kama hiyo bado ingekuwa kitendawili.
Tunajifunza nini kutokana na tukio la Sajuki?
Bado safari yetu ni ndefu sana kujikomboa kutoka mikononi mwa utumwa
uliotuzingira kwa sababu ya ubinafsi, wezi wanaodhulumu kazi zetu kwa
bei nafuu kwa kununua haki zetu hatuwaoni, ni kweli ilimpasa Sajuki
kuingia location ili apate fedha za matibabu? Kumbe wasanii
hawakopesheki jambo linaloashiri mwisho mbaya.

Ruge Mutahaba mratibu wa zoezi la kumchangia Sajuki.
Hatuwalaumu wasanii kwa kukosa fedha bali kwa kukosa umoja na kujenga
hoja au sera zinazoweza kuaminiwa na kuonyesha thamani yenu kwa ajili
ya kuwasaidia, mara nyingi usikika wasanii wakishirikiana na watu
maarufu au viongozi lakini hakuna msaada wa kudumu nahisi kuwa hakuna
mtu anayewa kutoa hoja na ukweli kuhusu maslahi ya jumla.
Leo hii katika tasnia ya filamu kuna taasisi mbili zinazohitaji
kuongoza wasanii kila unavyongea na upande mmoja kila mtu anajitahidi
kumlamu mwenzake wengi wanajiuliza malumbano haya ya Bongo Movie na TAFF
ni lini yataisha na kuwa wamoja watakaokaa na kujadili kwa kauli moja
na kusema biashara ya filamu iende hivi?
Yaliyojitokeza katika msiba ni aibu kuyasema lakini ilikuwa doa kubwa
kulisafisha yahitaji muda sana maana tulishuhudia watu wakipiga picha
au kutawala uongozi huku hata mitafaruku ikiendelea chini kwa chini kama
vile kutengenezwa Beji zilizotaka kutambulisha pande moja bila sababu
ya msingi, lakini pia wasanii kugombana kutokana na makundi hayo ni aibu
sana.
Hivi ni kweli unaweza kupendwa na mtu mwingine bila ya wewe kujipenda?
Hili tumeliona kwa Sajuki msanii anahitaji kupata fedha za matibabu
lakini ilikuwa ni utata hadi pale mtu anayelaumiwa kuingia na kufanya
harambe, kwa wasanii kubuni kitu chochote lakini haikutokea hivyo
wasanii waliojitokeza ni watatu tu, duh,,,
.

Stara alishiriki kuimba wimbo wa Mboni yangu kwa ajili ya kumchangia mumewe.
Binadamu kama binadamu hayupo aliyekamilika kwa asilimia mia moja,
lakini kama kuna mtu anaweza kufanya kazi au tukio la kijamii apimwe kwa
jambo hilo haina maana kuwa wasanii wote hawajielewi bali kuna wachache
wanaowapeleka wengine shimoni, tujadili kuhusu mustakabali wa tasnia ya
filamu Tanzania na wasanii wake.
Chanzo; filam central.
Asante!